SANAMU ZISIZONENA

Biblia kwa kina, Uncategorized 2 Comments

Shalom, jina la Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo lipewe sifa milele na milele, karibu tujifunze maandiko.

Biblia inasema katika [1 Wakorintho 12:2]..

1 Wakorinto 12:2 Mwajua ya kuwa MLIPOKIWA WATU WA MATAIFA, MLICHUKULIWA KUFUATA SANAMU ZISIZONENA, KAMA MLIVYOONGOZWA.  

Sanamu zisizonena zinazozungumziwa hapo sio kitu chochote kilichojiinua ndani ya mwanadamu kuliko Mungu hapana, bali ni zile sanamu zote zilizochongwa kwa kazi ya ufundi stadi wa mikono ya wanadamu na kisha kupambwa kwa dhahabu na fedha kwa lengo la kiibada, kuzihusianisha na Mungu, au kuziabudu kama mungu, na mfano wa sanamu hizi ni kama vile sanamu za ng’ombe, sanamu za tembo, sanamu za mabudha, sanamu za Mariamu au Yesu Kristo katika makanisa mfano kanisa katoliki, sanamu za miungu wanawake zenye mikono nane nane, kumi kumi, n.k, hizo ndizo sanamu zinazoongelewa hapo, ambazo ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu.


Ndugu, ikiwa unajiita mkristo na huku unaabudu hizo sanamu au kuzihusianisha na Mungu katika ibada zako, basi tambua kuwa wewe sio mkristo, ila unajidanganya na kujifurahisha tu mwenyewe katika udhalimu, kwa sababu hakuna sehemu yo yote ile biblia ilipoagiza mkristo kuchonga sanamu na kuisujudia au kuzihusianisha na ibada, unapofanya hivyo tambua kuwa, unamchukiza Mungu, unamchukiza Mungu unapoinama na kuzisujudia hizo sanamu zisizonena za budhaa, tembo, mariamu n.k na mwisho wa siku hutoweza ingia katika ufalme wa Mungu.

1 Wakorinto 6:9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, WALA WAABUDU SANAMU, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 

Bwana atusaidie kulifahamu hili.

Shalom 


Mada zinginezo

IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.


Kivipi Mungu ni Mungu wa miungu, je hao miungu ni masanamu?


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)

2 thoughts on - SANAMU ZISIZONENA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *