Nini maana ya mstari huu “unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu” (2 Petro 2:21) 

JIBU: Tusome..

2 Petro 1:21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. 

Katika mstari huo mtume Petro alimaanisha kuwa, maandiko yote matakatifu ya manabii wa Mungu hayakuandikwa kutokana na mitazamo yao binafsi au mawazo yao binafsi na mapendekezo yao binafsi, hapana! Bali waliandika yote wakiongozwa na Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani yao na si mapenzi yao, na ndio maana biblia inasema…

2 Timotheo 3:16  Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 

Neno lolote lililoandikwa na nabii Yeremia sio mawazo yake bali ni Roho wa Mungu, neno alilolosema nabii Mikaya kwa uweza wa Roho si lake bali ni Roho Mtakatifu, neno lolote lililoandikwa na nabii Zekaria sio mapendekezo yake bali ni Roho wa Mungu,  hivyo, endapo ukipuuzia maneno hayo katika maandiko matakatifu ni sawa na umempuuzia Mungu.


NI NINI TUNACHOPASWA KUKIFAHAMU HAPO?

Kitu tunachotakiwa kukifahamu hapo ni kwamba, ikiwa Roho Mtakatifu ndiye aliyewaongoza manabii wake hao watakatifu kuyaandika na kuyasema yote tunayoyasoma leo hii katika maandiko matakatifu (biblia ), basi, ni lazima pia tumuhitaji Roho Mtakatifu huyo huyo ili atufundishe, atueleweshe, atutafasirie, na kutufafanulia aliyoyasema Yeye Mwenyewe, vinginevyo hatutoweza elewa chochote. 


Wapo watu wanaojiita wakristo na kuamini katika biblia lakini wanampinga Roho Mtakatifu na karama zake katika kanisa, ila kinacho shangaza ni kuwa, wanataka wavielewe vile ambavyo vilisemwa na Roho Mtakatifu huyo huyo wanayempinga katika maandiko, hii inafurahisha sana. 

Wengine wanataka watumie sayansi zao ili kutafsiri kilichosemwa na Roho Mtakatifu katika maandiko, wengine wanataka kutumia elimu zao za falsafa (philosophy), na theologia (theology), walizosoma katika vyuo vya biblia ili kutafasiri maandiko, (ndugu sahau hicho kitu, na kama ulikuwa na mpango wa kwenda huko ni heri hiyo pesa uifanyie jambo la maana, Roho Mtakatifu hapatikani katika vyuo vya biblia), la sivyo utaishia kuona biblia inajichanganya tu, utaishia kuona Paulo anapingana na Musa, au nabii Yeremia anapingana na mtume Yohana, au mitume wanapingana na Yesu Kristo, kitu ambacho sio sahihi hata kidogo kwa sababu Roho aliyesema akiwa ndani ya Mwana wa Adamu, ndiye Roho aliyesema akiwa ndani ya mitume wake; Mfano, Bwana Yesu alisema…

Matayo 24:13  Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 

Harafu baadae unaona mitume Barnaba na Paulo wakiongozwa na Roho Yule Yule wakisema..

Matendo Ya Mitume 14:22  wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA NJIA YA DHIKI NYINGI.

Au nabii Yeremia anasema…

Yeremia 9:23 Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; 

24 bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana, 

Tena anakuja mtume Paulo akiongozwa na Roho huyo huyo anasema…

2 Wakorinto 10:17 Tena baadae mtume Paulo akiongozwa na Roho Huyo Huyo aliyekuwepo ndani ya nabii Yeremia anasema…. Lakini, Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana. 

Hivyo, ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu ili uweze kuyaelewa maandiko na kwamwe hutoona biblia ikijichanganya, na jinsi ya kumpata Roho Mtakatifu sio kwenda Seminary wala kwenye chuo cha biblia, bali ni kutubia na kuacha dhambi unazozifanya, acha hayo masanamu unayoyabusu na kuyasujudia, acha kuwaomba hao wafu unaowaita watakatifu, acha huo uasherati unaoufanya kwa siri, na kisha nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu (Matendo 2:38), vinginevyo utaishia Jehanam na hivyo vyeti vyako na PHD yako ya biblia.

Ufunuo 21:8  Bali waoga, NA WASIOAMINI, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. Hii ndiyo mauti ya pili. 

Na tena inasema..

Marko 16:16  AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA; ASIYEAMINI, ATAHUKUMIWA.

Bwana atusaidie sana, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

UKUMBUKE HUSIA WA BWANA.  

Ni maovu yapi yanayotoka kinywani mwa Bwana kulingana na (Maombolezo 3:38)


Ishara ya msalaba ni nini? Na je! Ni wapi biblia ilipoagiza mkristo kupiga ishara ya msalaba? 
 

Je! Ni lazima mgonjwa adongoke chini pale anapoombewa?


NENDENI MKAJIFUNZE MAANA YAKE MANENO HAYA ‘NATAKA REHEMA WALA SI SADAKA’


UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *