YEROBOAMU MWANA WA NEBATI.

Siku za Mwisho, Uncategorized No Comments

Jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo lipewe sifa milele na milele, leo kwa neema za Mungu tutamtazama na kujifunza kwa mfalme mmoja wa Israeli (mtumishi wa Mungu), aliyefahamika kama Yeroboamu Mwana wa Nebati, kwa sababu biblia inasema, mambo ya agano la kale yaliandikwa pia kama mifano ili kutuonya sisi watu wa sasa.


Kwa ufupi ni kwamba, Yeroboamu alikuwa ni mfalme wa kwanza wa Israeli (wa upande wa makabila kumi baada ya taifa hilo kugawanyika), mtu wa kabila ya Efraimu, hodari na shujaa, (1 Wafalme 11:28)

Mtu huyu wakati akiwa kijana kabisa, alipokea maono makubwa sana kutoka kwa Mungu kupitia nabii Ahiya, ya kuwa Mungu amemchagua ili kuwa mfalme juu ya makabilia kumi ya taifa la Israeli, atawale kama apendavyo yeye, lakini ilimradi tu atembee katika njia ya Bwana.

1 Wafalme 11:29 Ikawa zamani zile Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya, Mshiloni, alikutana naye njiani; naye Ahiya amevaa vazi jipya, na hao wawili walikuwa peke yao mashambani. 

30 Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili. 

31 Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi, 

Na Kweli baada ya kipindi kirefu sana kupita, neno la Bwana likatimia juu yake kama nabii wa Bwana Ahiya alivyosema, na Yeroboamu akatawala juu ya makabila kumi na mawili ya Israeli. 

Lakini mtu huyu alimuasi Mungu na kuwakosesha watu wa taifa hilo kwa kuwatengenezea ng’ombe wawili wa dhahabu na kuwaambia watu hao, hii ndio miungu yenu iliyowatoa misri, akaamuru sikukuu za kushika na kwenda kutoa dhabihu kwenye madhabahu ya ng’ombe hizo alizozitengeneza. 

1 Wafalme 12:28 Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng’ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.

 29 Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani.

30 Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani.

31 Tena akafanya nyumba za mahali pa juu, akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani.

 32 Yeroboamu akaamuru kushika sikukuu katika mwezi wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi, mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda, akapanda juu ili kuiendea madhabahu. Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea dhabihu wale ng’ombe aliowafanya; akawaweka katika Betheli wale makuhani wa mahali pa juu alipokuwa amepafanya. 

Mtumishi huyu wa Mungu Yeroboamu (mfalme), alifanya hivyo kutokana na kuogopa kuwa, endapo angewafundisha au kuwaambia watu kuenenda katika njia sahihi ya Mungu (kwenda kuabudu Yerusalemu), basi angeupoteza ufalme, kitu ambacho sio sahihi hata kidogo, kwani Mungu alishamwambia kuwa, endapo atayashika yote aliyomuuru, basi Bwana angekuwa pamoja naye siku zote na angeifanya nyumba yake kuwa imara zaidi (1 Wafalme 11:38), lakini yeye alifanya kinyume chake

1 Wafalme 12:26 Yeroboamu akasema moyoni mwake, BASI UFALME UTAITUDIA NYUMBA YA DAUDI.

 27 Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda.

 28 Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng’ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. 

Umeona hapo?..mtumishi huyu wa Mungu mfalme Yeroboamu aliamua kuwakosesha watu kwa makusudi kabisa, na huku akitambua kuwa, anachokifanya si sahihi na ni makosa mbele za Mungu?


Sasa tabia hii ya Yeroboamu mwana wa Nebati ndiyo inayoendelea sasa hivi katika siku hizi za mwisho miongoni mwa watumishi wengi sana wa Mungu, ambao wengi wanapewa na walipewa maono makubwa tangu ujana wao kama Yeroboamu, wengine karama na vipawa, wengine Bwana alisema nao kwa njia mbali, wengine Bwana aliwatokea na kujidhihirisha kwao, lakini pale Mungu anapowafikisha hatua fulani katika utumishi, wanaanza kuwapostosha watu kwa kuwafundisha uongo kutokana na hofu za kupoteza sifa au umaarufu, kama tu ilivyokuwa kwa Yeroboamu mwana wa Nebati alivyowaza kupoteza ufalme, wanasahau kuwa waminifu kwa Mungu na kudumu katika kweli Yake kama Yeroboamu, wanaanza kuwaaminisha watu kuwa, kuishi na binti au kijana msiyefunga nae ndoa haina tatizo sana, kuzikiliza miziki ya kidunia sio dhambi kubwa kiivyo.., uvaaji suruali, vimini, na nguo zinazochora maungo ya mwanamke havina shida sana Mungu anatazama roho, wanawake kufunika vichwa wakati wa ibada ni uzamani, binti kujipamba haina shida, kijana wa kiume nyoa kiduku, vaa modo, na njoo tu kanisani hakuna shida tunaishi kwa neema, jisikie huru, kijana chora tattoos, vaa heri kama mwanamke, fuga rasta, uza pombe na sigara hakuna shida, ubatizo sio kitu cha maana sana.., na mambo mengine kama hayo pasipo kujua kuwa, kwa kufanya hivyo nafsi nyingi za watu zinapotea kila siku Jehanam. 


Mpendwa, ikiwa Bwana amekupa kibari kama hicho huna budi kusimama katika neno lake na uwe mwaminifu, haijalishi hata kama watu wote watakuwa kinyume chako kama nabii Yeremia, simama katika njia ya Bwana, waambie watu ukweli, usiende kulia wala kushoto, na ndivyo itakavyokua faida kwako.

Matayo 24:45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?

46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 

47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zingizeno

KWA SABABU NALIWAOGOPA WALE WATU, NIKATII SAUTI YAO. 

Tabia moja ya unafiki unayopaswa kuiepuka.


USIMLAANI MKUU WA WATU WAKO.


Je! Umeiamini Injili Ipi?


Unaweza kunitajia kanisa la kweli siku hizi za mwisho?


Ni mambo ya nyumba ipi ambayo mfalme Hezekia aliambiwa kuyatengeneza? (Isaya 38:1)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *