Tabia moja ya unafiki unayopaswa kuiepuka.

Biblia kwa kina, Uncategorized No Comments

Moja ya tabia ambayo Bwana Wetu Yesu Kristo aliikemea sana na kutukataza tusiwe nayo ni unafiki, tunaliona hilo sehemu kadha wa kadha kwenye maandiko matakatifu aliposema kuwa, katika kuishi kwetu na kuendenda kwetu tusiwe kama wanafki, tunapotoa sadaka tusiwe kama wanafiki, tusalipo tusiwe kama wanafiki, tufungapo tusiwe kama wanafiki, na sehemu nyingine nyingi mno alipoikemwa tabia hiyo ya unafiki na watu wanafiki.

Matayo 6:5 Tena msalipo, MSIWE KAMA WANAFIKI; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 

Hii inatufundisha kwamba, unafiki ni moja ya tabia mbaya sana ambayo Bwana Wetu Yesu Kristo hapendezwi nayo hata kidogo. 


Leo tutatazama tabia moja ambayo ukiiona hiyi ipo ndani yako, basi tambua kuwa, wewe ni mmoja wapo wa WANAFIKI mbele za Mungu hivyo fanya hima uiepuke haraka sana. Tabia yenyewe ni pale baadhi ya watu unapowafuata na kuwaambia habari za wokovu wa roho zao uliopo Katika Yesu Kristo, utakuta mtu huyo anakujibu, “BABU YANGU, BABA YANGU NA MAMA YANGU WOTE NI WATU WA DINI HII AU DHEHEBU HILI, HIVYO, HUWEZI NIAMBIA CHOCHOTE KILE KUHUSU DINI YANGU HII AU DHEHEBU LANGU HILI” au “MIMI NIMEZALIWA KATIKA DHEHEBU HILI, HIVYO NITAKUFA KATIKA DHEHEBU HILI”,  


Ndugu, ukijiona wewe ni mmoja wapo wa watu wenye tabia hiyo, basi tambua kuwa wewe ni mnafiki mkubwa sana kwa sababu, kama unapoletewa habari za Mungu labda ubatizo sahihi wa kwenye maandiko, unaanza kusema “mimi ni mpentekoste au mkatoliki au mluthelani nitakufa katika dhehebu langu hili”..mbona sasa babu yako na baba yako ni watu maskini na mafukala na husemi kuwa na wewe UTAKUFA KATIKA UMASKINI NA UFUKARA HUO HUO?..Badala yake unapambana juu chini ili uepukane nao? Kwa sababu, ilikupasa pia mtu anapokuletea taarifa ya nafasi za kazi umjibu kuwa “babu yangu ni fukara, baba yangu ni fukara, na mimi pia nitakufa katika ufukara wetu huu huu, hivyo huwezi niambia kitu chochote kuhusu ufukara wetu”. Mbona husemi hivyo unapoletewa taarifa ya kazi na fursa mbali mbali? Huo ni unafiki mkubwa sana unaotakiwa kuuepuka.


Unapaswa utambue kwamba, wewe, babu yako, na baba yako na hilo dhehebu lako, ambalo unasema utakufa katika hilo, hamtakuwa na udhuru siku ile mnapokataa sasa habari njema ya wokovu mnayoletewa na kuidharau leo hii, hamtakuwa na udhuru wewe na hilo dhehebu lako unapoambiwa kuabudu sanamu na kuwaomba watu walio kufa ni dhambi na unakataa, hautakuwa na udhuru wewe na baba yako unapoambiwa ubatizo sahihi ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo na unakataa, hautokuwa na udhuru wewe na askofu wako unapoambiwa hakuna askofu wala mchungaji mwanamke na unanakataa, hutokuwa na udhuru wewe na nabii wako unapoambiwa kuvaa nusu uchi na suruali kwa wanawake ni dhambi na unakataa, hutokuwa na udhuru kwa kusema kanisa letu lina utaratibu huu na linaamini hivi, hivyo nitakufa katika dhehebu langu hili, hutokua na udhuru kabisa kwa huo UNAFIKI WAKO.

Yohana 15:22 KAMA NISINGALIKUJA NA KUSEMA NAO, WASINGALIKUWA NA DHAMBI; LAKINI SASA HAWANA UDHURU KWA DHAMBI YAO.

Na Wanafiki wote wenye tabia kama hiyo kwao kitakuwa ni kilio na kusaga meno baada ya hukumu..

Matayo 24:51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake PAMOJA NA WANAFIKI; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 

Hivyo, kama unavyofanyia kazi taarifa za fursa za kazi na ajira unazoletewa, na tena bila kujali kama umezaliwa katika familia maskini, ya kikulima, au ya kitajiri, ndivyo vivyo hivyo pia unavyotakiwa kufanyia kazi taarifa za habari ya wokovu unazoletewa, bila kujali dini yako au hilo dhehebu lako ulilozaliwa nalo, vinginevyo utakuwa mnafiki tu mbele za Bwana.

Bwana atupe kulitambua hilo.

Tafadhari Washirikishe na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)


Ni thawabu gani inayozungumziwa katika (Mathayo 6:16)?


Bwana wa mavuno ni nani? (Mathayo 9:38)


Ishara ya msalaba ni nini? Na je! Ni wapi biblia ilipoagiza mkristo kupiga ishara ya msalaba? 


IJAPOKUWA NALIWAUZUNISHA KWA WARAKA ULE, SIJUTI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *