Bwana wa mavuno ni nani? (Mathayo 9:38)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

JIBU: Tusome…

Matayo 9:37 Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. 

38 Basi MWOMBENI BWANA WA MAVUNO, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. 

Kwanza hadi anaitwa Bwana wa mavuno maana yake ni kuwa, anao watendaji kazi ambao kazi yao ni hiyo ya uvunaji, hivyo, hao watenda kazi wote ambao ni wavunaji, Bwana wao ndiye huyo anayeitwa Bwana wa Mavuno. 

Sasa Bwana wa mavuno huyu ni nani? Bwana wa mavuno si mwengine zaidi ya Yesu Kristo,

Ufunuo 14:14  Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.

15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, AKIMLILIA KWA SAUTI KUU YEYE ALIYEKUWA AMEKETI JUU YA LILE WINGU, TIA MUNDU WAKO, UKAVUNE; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. 

Yesu Kristo kama Bwana wa mavuno, anawatuma wavunaji wake (watumishi wake) kwa kazi mbali mbali za uvunaji, na watumishi wake ambao wanafanya hiyo kazi ya uvunaji wapo katika makundi mawili. 

Kundi la kwanza: Watumishi wanadamu.

Hawa ni wale wote wanaoifanya kazi ya Mungu ya kuwavuna watu kutoka shambani (ulimwenguni au gizani) na kuwaleta kwa Kristo, watu hawa wanahubiri habari njema ya wokovu na wamepewa mamlaka juu ya nguvu zote za giza katika shughuri yao ya uvunaji watu ulimwenguni (gizani)

Luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. 

Kundi la pili: Watumishi Malaika 

Matayo 13:39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; NA WALE WAVUNAO NI MALAIKA. 

Kundi hili la wavunaji hufanya kazi mwisho wa dunia (pale mtu anapokufa) na siku ile ya kiyama. Mtu anapokufa sasa, iwe katika dhambi au utakatifu, watumishi hawa malaika huja na kumpeleka mtu huyo sehemu husika, kama ni peponi au jehanamu ya moto, na katika siku ya mwisho wa dunia pia, watafanya kazi hii hii ya uvunaji kwa kupokea amri na mamlaka kutoka kwa Mvunajii mkuu.

Je! Umeshatubu dhambi zako kwa kumwamini Bwana Yesu na kubatizwa katika ubatizo sahihi? Kama hujafanya hivyo, basi amua sasa kwani bado hujachelewa, tubu kwa kuaamisha kuacha dhambi zako na kuitii injili ya Bwana wa Mavuno iliyohubiriwa na wavunaji wake wanadamu (mitume na manabii) dini yako au dhehebu lako halitoweza kukupa wokovu kama usipotaka kumtii Bwana wa mavuno na injili yake, biblia ipo wazi kabisa kuwa, wote wasio itii injili ya Kristo wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele katika like ziwa la moto.

2 Wathesalonike 1:8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao WASIOITII INJILI YA BWANA WETU YESU; 

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; 

Hivyo, acha ibada za sanamu na wafu, acha kuvaa nusu uchi na masuruali, acha usengenyaji na umbea, acha udunia na miziki ya kudunia na uitii injili kabla hujaamgamia milele na milele kwenye ziwa la moto.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu

Bwana akubariki, shalom.

 +255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo

Waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 

Ishara ya msalaba ni nini? Na je! Ni wapi biblia ilipoagiza mkristo kupiga ishara ya msalaba? 

JE! KUNA TOFAUTI GANI KATI YA MTU WA MUNGU NA MTOTO WA MUNGU?


Je! Ni sawa kuwa na sala au maombi maalum kwa Malaika fulani kibiblia?


Ni hukumu ipi ya Ibilisi inayozungumziwa katika Waraka wa (1 Timotheo 3:6?)

LEAVE A COMMENT