Ni thawabu gani inayozungumziwa katika (Mathayo 6:16)?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized


Tusome…

Matayo 6:16  TENA MFUNGAPO, msiwe kama WANAFIKI wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, WAMEKWISHA KUPATA THAWABU YAO.

Ili tueleweni ni thawabu gani au ni thawabu ya nini inayozungumziwa hapo, kwanza inabidi tuelewe nini maana ya thawabu.

Thawabu ni malipo ambayo mtu anayapata kutokana na jitihada alizozifanya au kitu alichokifanya kwa ajili ya jambo fulani.

Hivyo, Bwana Yesu aliposema mfungapo msiwe kama WANAFKI, harafu anasema, Amin nawaambia wamekwisha kupata thawabu yao, maana yake ni kwamba, wamekwisha kupata hiyo thawabu yao ya UNAFKI au kwa lugha rahisi ni kuwa, watapata malipo ya huo UNAFKI WAO. Huwezi fanya jambo kwa unafki harafu utegemee baraka kutoka kwa Mungu kwa ajili ya jambo hilo, hicho kitu hakipo, kwani biblia inasema Mungu hadhihakiwi, utakacho panda ndicho utakacho vuna..

Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; KWA KUWA CHO CHOTE APANDACHO MTU, NDICHO ATAKACHOVUNA. 

Ikiwa bado hujampa Bwana maisha yako, basi tambua kuwa, muda haupo upande wako, huna garantii ya maisha yako, muda wowote na wakati wowote kifo kinaweza kukupata, hivyo ukifa katika dhambi na hujampokea Kristo, safari yako ni moja kwa moja jehanamu, basi amua leo ndani ya moyo wako kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kumpokea Kristo na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ikiwa utapenda kumpa Kristo leo maisha yako, basi tafuta kanisa lolote lile la kiroho lililopo karibu nawe au wasiliana nasi kwa namba hizi kwa msaada.

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.


Mada zinginezo:

UNAKO BISHA HODI NDIKO UTAKAKO FUNGULIWA, UNACHOKITAFUTA, NDICHO UTAKACHOKIONA


UMEPATA FAIDA GANI?


Bwana alimaanisha nini katika  (Mathayo 24:46)?


Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)


TAFAKARI KWA KINA HATIMA YA UNACHOKIFANYA ILI MUNGU ASEME NA WEWE.


JINSI AMRI YA UPENDO INAVYOWAFANYA WATU WADUMU KATIKA DHAMBI

LEAVE A COMMENT