UNAKO BISHA HODI NDIKO UTAKAKO FUNGULIWA, UNACHOKITAFUTA, NDICHO UTAKACHOKIONA

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Biblia inasema katika…

Matayo 7:7  Ombeni, nanyi mtapewa; TAFUTENI, NANYI MTAONA; BISHENI, NANYI MTAFUNGULIWA; 

8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; NAYE ABISHAYE ATAFUNGULIWA. 

Ikimaanisha kuwa endapo mtu akidhamiria moyoni mwake kupata kitu chochote kile kwa bidii na kwa njia yoyote ile, basi atakipata tu, mfano; leo hii kijana akidhamiria kupata labda utajiri hata kwa njia kuabudu shetani na kafara, huyo ataupata tu, au binti akidhamiria kupata pesa hata kwa njia ya kufanya ukahaba n.k  ataipata tu, kwa sababu ndivyo ilivyo, ukiweka nia ya kupata kitu fulani kwa njia yoyote ile, bila kujali gharama na hasara utakayoipata, basi, utakipata tu.

Lakini yote kati ya yote, Bwana Yesu alitupa shauri la wapi pa kubisha, nini cha kufanya, na nini cha kutafuta, alisema…

Matayo 6:33  Bali UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 

Ikiwa tutadhamiria ndani ya mioyo yetu kuutafuta huu ufalme wa Mungu wa milele, na kubisha huko bila kujari gharama na hasara, basi, tutaupata na tutafunguliwa, matendo yetu na jitihada zetu za kuutafuta ufalme ndio yatakayotuwezesha. 

Lakini ndugu, ukiona jitihada zako na matendo yako si yale ya kubisha na kuutafuta ufalme wa Mungu, basi fahamu kuwa, kuna SEHEMU NYINGINE UNAYOITAFUTA NA KUBISHA HODI HUKO (nayo si nyingine zaidi ya jehanamu na baadae kutupwa katika ziwa la moto na kiberiti) hakika utapaona na kufunguliwa huko


Sasa yafuatayo ni baadhi ya matendo machache sana, ambayo yanaashiria kuwa, unaitafuta jehanamu ya moto na kubisha hodi huko.

       1. IBADA ZA WAFU

Ukijiona hadi leo hii unawaomba marehemu (watu waliokufa) mfano; Paulo, Petro, Yasinta, Teresa, mtakatifu Rita n.k badala ya Yesu Kristo, au unafanya vyote kwa pamoja, yaani unawaomba watu waliokufa tayari na kumwomba Yesu Kristo pia, basi fahamu kuwa, unaitafuta Jehanamu na kubisha huko ndugu na baadae utatupwa kwenye ziwa la moto na kiberiti usipotaka kuacha kwani biblia ipo wazi kabisa…

Kumbukumbu La Torati 18:10  Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE  WAFU

12 KWA  MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 

Na WACHUKIZAO wote sehemu yao ni katika ziwa la moto (ufunuo 21:8)

       2. MAPAMBO NA FASHION.

Binti/mama, ukijiona unapenda kujichubua, make ups, lipstick, nywele bandia, kope bandia, kucha bandia, OLE WAKO WEWE kwa sababu unashindana na Muumba Wako aliyekuumba katika ukamilifu ( Isaya 45:9), ukijiona unapenda kutembea nusu uchi barabarani, mapaja wazi, kifua chako wazi na tight zinazochola maungo yako, basi  fahamu unaitafuta jehanamu na unabisha huko, kwani unawafanya watu wanao kutazama na kukutamani wazini mioyoni mwao na kwenda jehanamu wasipotubu na OLE wake wewe uliyewakosesha.

Marko 9:42 Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. 

      3. UONGO, MATUSI, NA USENGENYAJI

Huo uongo unaousema kila siku kwa marafiki zako, ndugu zako na kazini kwako, hayo matusi yanayotoka kinywani mwako ukidhani ndio ujanja, na uhodari, huo usengenyaji wako kwa majirani zako na ndugu zako, jua kuwa, unakonga hodi jehanamu na utafunguliwa tu usipotaka kutubu

Matayo 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 

Mengine, ni uzinzi, ulevi, uchawi, kwenda kwa waganga, ibada za sanamu, utoaji mimba, utazamaji wa picha za ngono, miziki ya kidunia, night clubs n.k 

Hivyo, ukijiona wewe ni mmoja wapo wa hayo, basi, huna budi kuacha leo na kumpa Kristo maisha yako, kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji tele na kwa JINA LA YESU KRISTO (matendo 2:38) na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye atakufundisha yote na kukufanya uishi maisha ya kumpendeza Mungu kila siku ili usibishe hodi tena Jehanamu

Bwana akubariki, shalom.

+255652274252/ +255789001312


MADA ZINGINEZO:

Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?


Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?


Kwanini Bwana alisema ‘Ninyi ni chumvi ya dunia’?


VIFUNGO VYA WOTE VIKALEGEZWA.


Mbegu iharibikayo ni ipi? (1 Petro 1:23)


NAO WATAJIEPUSHA WASISIKIE YALIYO KWELI


Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?

One Reply to “UNAKO BISHA HODI NDIKO UTAKAKO FUNGULIWA, UNACHOKITAFUTA, NDICHO UTAKACHOKIONA”

LEAVE A COMMENT