Kwanini Sanduku la Mungu lilitwaliwa na Wafilisti huko shilo? (1 Samweli 4:11)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Kwanini sanduku la Mungu, mahali ambapo Mungu aliweka jina lake lilitwaliwa na wafilisti huko shilo?


JIBU: Si kwamba sanduku la Mungu pekee lilitwaliwa na wafilisti huko shilo, hapana! Bali Wafilisti pia waliwapiga Waisraeli vibaya sana na kila mmoja alikimbia hemani mwake, na si hivyo tu, pia Waisraeli wengi sana waliuwawa huko shilo, wakiwemo na watoto wawili wa Eli japokuwa sanduku la Mungu mahali ambapo Mungu aliliweka jina lake lilikuwepo hapo,  walipigwa na hilo sanduku lao la agano la Mungu walilolitumainia likachukuliwa, kitu ambacho si cha kawaida kabisa. 

1 Samueli 4:10 Wafilisti wakapigana nao, ISRAELI WAKAPIGWA, WAKAKIMBIA KILA MTU HEMANI MWAKE; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu.

 11 HILO SANDUKU LA MUNGU LIKATWALIWA; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa. 

Lakini, si kwamba Mungu alishindwa kuwapigania Waisraeli na kulilinda sanduku la agano kama alivyokuwa akifanya sehemu zingine, la hasha! Bali ni yeye Mwenyewe kabisa Ndiye aliyeruhusu hayo yote yatokee kwa kusudi au lengo maalamu, kwani hakuna taifa, mji, au nchi yoyote ile inayopatwa na hali mbaya ambayo Mungu hajairuhusu (lakini anafanya hivyo kwa sababu maalumu)

Amosi 3:6 Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? MJI UTAPATIKANA NA HALI MBAYA, ASIYOILETA BWANA?

Umeona?….Hivyo, kitendo cha Mungu kuruhusu Waisraeli kupigwa na sanduku kutekwa huko shilo, kilikuwa na sababu maalumu, na sababu yenyewe si nyingine zaidi ya dhambi za taifa hilo ambazo walizokuwa wakizitenda mbele za Mungu 

Yeremia 7:12 Lakini enendeni sasa hata mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, MKAONE NILIVYOPATENDA KWA SABABU YA UOVU WA WATU WANGU ISRAELI.

Wana Waisraeli walikuwa wakitenda dhambi na huku wakitumainia sanduku la Mungu, mahali ambapo Mungu ameliweka jina lake, wakidhani kwa njia hiyo Mungu atawaachilia tu hata kama wakitenda uovu kitu ambacho sio sahihi, Mungu hapendezwi na dhambi hata kama ameliweka jina lake mahali fulani, Hicho kitu hakipo kabisa.


Sasa tabia hii ndiyo inayoendelea leo hii ndani ya kanisa la Mungu miongoni mwa watakatifu.

Kumbuka; wale wote waliomwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika jina lake sawasawa na (matendo 2:38), hao pia ni WaIsraeli rohoni, uzao wa Ibrahimu, kwa njia ya imani (Wagalatia 3:7), Na nyumba ya Mungu ambayo anakaa ndani yake sio kwenye sanduku tena wala hekalu bali kwenye miili yetu, hiyo ndio nyumba yake, hekalu la Mtakatifu wa Israeli, Mungu Aliye hai.

1 Wakorinto 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

Na tena biblia inatuonya kuwa, mambo hayo yailiyotokea katika agano la kale, yaliandikwa kwa jinsi ya mifano ili kutuonya sisi ili tusiwe kama wao

1 Wakorinto 10:11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 

Lakini sasa hivi imekuwa kinyume chake wala hatukumbuki na hatutaki kujifunza kwa mifano hiyo iliyoandikwa, kwa sababu tu Mungu yupo ndani yetu na anajidhihirisha katika makusanyiko yetu, basi hatuogopi kutenda dhambi, mpendwa, sio kwa sababu Mungu anatenda kazi ndani yako basi ndo umepata kibali cha kuishi maisha ya dhambi, sio kwa sababu unatoa mapepo au unanena kwa lugha, ndio umepata kibali cha kuishi unavyotaka, sio kwa sababu unaona maono na kuota ndoto, au kwa sababu wewe ni askofu au shemasi ndio umepata hidhini ya kudanganya, si kweli hata kidogo, acha dhambi, acha kudanganya, acha kutukana, acha udunia kijana, acha kuvaa kikahaba mwanamke Mkristo, acha umbea na usengenyaji, acha uchawawi kama Baalamu, acha anasa za dunia hii, acha miziki ya kidunia, acha kutazama picha chafu za ngono kisiri siri, acha pombe na uasherati, tubu na wala usitumainie uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako, ishi maisha ya utakatifu mbele za Mungu, wakumbuke Waisraeli na sanduku lao huko shilo, vinginevyo utaishia kukataliwa.

Yeremia 7:14 BASI, NITAITENDA NYUMBA HII, IITWAYO KWA JINA LANGU, MNAYOITUMAINIA, na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu, kama nilivyopatenda Shilo. 

Bwana atusaidie, Shalom.

Tafadhari, washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

USITUMAINIE HEKALU LA BWANA


Makuhani wa Mungu ni watu gani katika biblia?


MCHUNGAJI WAKO NI NANI?


Pazia la Hekalu ni nini katika biblia?


NENDENI MKAJIFUNZE MAANA YAKE MANENO HAYA ‘NATAKA REHEMA WALA SI SADAKA’


Mana ni nini katika maandiko?

LEAVE A COMMENT