Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

JIBU: Tusome 

2 Wafalme 18:1 Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia, mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala. 

2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria. 

3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya Daudi, baba yake. 

4 Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; AKAIVUNJA VIPANDE VIPANDE ILE NYOKA YA SHABA ALIYOIFANYA MUSA; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; NAYE AKAIITA JINA LAKE NEHUSHTANI

Nehushtani Maana yake ni Kipande cha shaba. 

Sababu ya mfalme Hezekia kuiita NEHUSHTANI (yaani kipande cha shaba), ile nyoka ambayo Musa aliifanya kule jangwani, ni kuonesha kuwa, hakukuwa na nguvu yo yote ile tena katika yule nyoka wa shaba kwa wakati ule, kwa sababu wana wa Israeli hadi wakati huo kwa kukosa ufunuo, walikuwa bado wakiiabudu na kuifukizia uvumba (Machukizo kwa Bwana Mungu).

2 Wafalme 18:4 Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; MAANA HATA SIKU ZILE WANA WA ISRAELI WALIKUWA WAKIIFUKIZIA UVUMBA; naye akaiita jina lake Nehushtani 

Mfalme Hezekia aliiita hivyo kuonesha kuwa, hakukuwa na utofauti wo wote ule kati ya nyoka huyo wa shaba na vipande vingine vya shaba vilivyokuwapo tu wakati huo, hivyo akaiita ile nyoka ya shaba NEHUSHTANI, yaani KIPANDE CHA SHABA, kumaanisha kwamba, wana wa Israeli walikuwa wakiabudu kipande cha shaba (NEHUSHTANI), isiyoweza sikia wala kuona, isiyoweza kuokoa wala kujiokoa, kwa sababu haikuweza kusimama mbele ya mfalme Hezekia ambaye alikuwa ni mwanadamu tu, pale alipoivunja vunja vipande vipande. 


Hii ikifunua pia, Sanamu yo yote ile ya shaba, iwe ya mwanawake mwenye mikono kumi kumi au nane nane, iwe ya buza, mariamu, yesu, tembo, ng’ombe n.k, nazo ni NEHUSHTANI TU (YAANI NI VIPANDE VYA SHABA TU KAMA VILIVYOVIPANDE VINGINE VYA SHABA), hupaswi kuviinamia na kuvisujudia, wala hupaswi kuvifukizia chochote kile.


Sanamu lo lote lile la mti, liwe la buza, la yesu, tembo, au ng’ombe n.k, hicho ni KIPANDE CHA MTI TU KAMA ILIVYOKUWA KWA VIPANDE VINGINE VYA MITI), hupaswi kuliinamia wala kulisujudia, wala kulifukizia chochote kile (hayo ni machukizo kwa Bwana). 

Kutoka 20:4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 

USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA; kwa kuwa Mimi, Bwana, Mungu wako,ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 

Wapo watu leo hii kwa kukosa ufunuo wa maandiko, wanajikuta wakisujudia masanamu pasipo kujua, na wengine hata kuzifukizia uvumba kwa kisingizio hicho cha nyoka wa shaba, mpendwa, nyoka ya shaba haipo tena, ilishavunjwa vunjwa vipande vipande miaka mingi sana huko nyuma na mtiwa mafuta wa Bwana (mfalme Hezekia), na Kitendo hicho cha Musa kumuimua nyoka wa shaba hakikumaanisha na wewe ukachonge sanamu na kulibusu na kuliinamia na kulisujudia, bali kilikuwa kinamfunua Mwana Wa Adamu.

Yohana 3:14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 

15 ILI KILA MTU AAMINIYE AWE NA UZIMA WA MILELE KATIKA YEYE. 

Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka wa shaba, ndivyo Kristo naye alivyoinuliwa pale msalabani, na kama vile ilivyokuwa kwa wale wote waliong’atwa na nyoka walivyopata uzima baada ya kumtazama yule nyoka wa shaba, ndivyo ilivyo na wote waliong’atwa na nyoka ( yaani dhambi), watakapopata Uzima pindi watakapomtazama Mwana wa Mungu.


KUMBUKA: Kule jangwani hakuna mtu aliyelazimishwa kumtazama yule nyoka ili awe na uzima, la hasha! Bali mtu binafsi alipoona kuwa anayo haja ya uzima wake, alifanya hivyo, ndivyo ilivyo na sana, hakuna mtu anayekulazimisha kumtazama na kumgeukia Kristo, bali kama unaona unayo haja ya uzima wako (ambao ni wa milele), basi mtazame Kristo sasa, kwa kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuziacha kabisa, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu atakayekuwezesha kudumu katika injili iliyohubiriwa na mitume na manabii watakatifu.

Matendo 2:38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTOMPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Ni mambo ya nyumba ipi ambayo mfalme Hezekia aliambiwa kuyatengeneza? (Isaya 38:1)


TOKA KATIKA NYUMBA ZA MAKAHABA


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.


NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.


Nini maana ya mstari huu? “Na amani ya Kristo iamue miyoni mwenu” (Wakolosai 3:15)

LEAVE A COMMENT