Je! Mtu anaweza kuwa na kipawa cha Mungu kabisa na Bado akawa mtumishi wa uongo?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Je! Mtu anaweza kuwa na kipawa cha Mungu kabisa na bado akawa mtumishi wa uongo?


Jibu ni ndio, mtu anaweza akawa na kipawa cha Mungu kabisa na bado akawa mtumishi wa uongo na kuwapeleka watu wengi tu kuzimu kwa kuwadanganya na kuwafundisha Injili nyingine kabisa tofauti na ile iliyohubiriwa na mitume na manabii.

Mtu anaweza akawa mtume, nabii, mchungaji, mwinjilisti au mwalimu kwa uweza wa Mungu kabisa na bado akawa mtumishi wa uongo kwa kulichanganya neno la Mungu na uongo kwa sababu maandiko yanasema, kama vile Mungu alivyotoa vipawa kwa watumishi wake wa kweli na wanaosimama katika kweli ya neno.

Waefeso 4:8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. 

9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?

10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.

11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 

Ndivyo pia alivyotoa vipawa hivyo vya utume, unabii, uinjilisti, uchungaji na ualimu kwa watumishi wa uongo ambao ni WAKAIDI WA NENO LA MUNGU, wanaohubiria watu mafanikio ya dunia hii tu na si kuwaandaa watu kukutana na Bwana wao na siku ya hukumu.

Zaburi 68:18 Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; NAAMHATA NA WAKAIDI, Bwana Mungu akae nao. 

Hivyo basi, usipumbazwe na kipawa cha mtu ye yote yule kwani hivyo hata WAKAIDI WANAPEWA, usiseme huyu ni Mwinjilisti mkubwa, au mtume mkubwa, au mwalimu mkubwa au mchungaji maarufu ukadhani ni mtumishi wa Mungu, ndugu utapotea nae siku ya hukumu, wewe tazama neno la Mungu linasema nini, huyo mtumishi wako si mkubwa kiliko neno.


Na Ukiona hakuhubiri kuacha kuvaa hivyo vimini na visuruali vyako wewe mwanamke, tambua kuwa huyo ni kaidi wa injili ya Kristo (mtumishi wa uongo tu), ukiona hakuambii kuacha hayo manywele yako bandia, mawigi, rasta, make up, lipstick, hereni, mikifu na vikuku, basi tambua kuwa huyo ni kaidi tu wa injili ya Kristo aliyepewa hicho kipawa (mtumishi wa uongo), ukiona unahubiriwa injili na uambiwi chochote kuhusu kwenda kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kama maandiko yanavyosema, basi tambua kuwa huyo mtumishi ni kaidi tu aliyepewa kipawa (mtumishi wa uongo). Ukiona anakuruhusu wewe mwanamke kuwa askofu au askofu msaidizi, anakuruhusu wewe mwanamke kuwa mchungaji au mchungaji msaidizi, tambua kuwa, huyo ni kaidi tu aliyepewa kipawa (mtumishi wa uongo). Ukiona hakuambii kufunika hicho kichwa chako Mwanamke uombapo, basi tambua huyo ni kaidi tu, na ukimfuta mwisho wa siku wote mtaishia jehanamu ya moto.

Unachopaswa kufanya ni kurejea hiyo biblia yako na udumu katika injili iliyohubiriwa na mitume na manabii (maandiko matakatifu), usiyumbishwe na umaarufu wa mtumishi yo yo yule, wala miujiza, wala vipawa, kwani hivyo hata wakaidi wanapewa.

Zaburi 68:18 Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; NAAMHATA NA WAKAIDI, Bwana Mungu akae nao. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.


VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE.


Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)


JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?

LEAVE A COMMENT