WEMA NA UVUMILIVU WA MUNGU 

Biblia kwa kina, Uncategorized No Comments

Katika maisha tunayoishi, kila mtu anauona wema wa Mungu ambao haujifichi, haijalishi kama huyo mtu maisha yake ni ya dhambi na anasa, au ni ya haki na utakatifu, makundi hayo yote ya watu yanauona wema wa Mungu kwani wote anatupa afya, wote anatupa pumzi na uhai, wote tunaoa na kuolewa, wote tunapata watoto, na ndio maana maandiko yanasema

Mathayo 5:45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; MAANA YEYE HUWAANGAZIA JUA LAKE WAOVU NA WEMAHUWANYESHEA MVUA WENYE HAKU NA WASIO HAKI.

Lakini hayo yote ukiwa nayo, haimaanishi kwamba wewe ni wakupendeza sana machoni pa Mungu, na wala sio kwamba wewe ni wa kuvutia sana mbele za Mungu, unatenda dhambi, mwabudu Sanamu, mwenda kwa waganga, mlevi, mzinzi na mwasherati, huna upendo, unavaa mavazi ya kikahaba kama suruali na vimini Mwanamke, ni mchawi, unaapa kwa uongo, n.k lakini Mungu kwa wema wake amekupa afya uliyonayo na umeamka salama kabisa, amekupa watoto, mume, mke n.k. Tambua kuwa, anachotaka kutoka kwako ni wewe ugeuke katika njia zako mbaya na umrudie Yeye, hiyo pumzi aliyokupa asubuhi hii ya leo kwa wema wake ni ili umgeukia kwa kutubu.

Warumi 2:4 Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa WEMA WA MUNGU WAKUVUTA UPATE KUTUBU?

Umeona hapo?..lengo la huo wema wa Mungu na uvumilivu wake kwetu ni ili sisi tuifikie toba, na si kitu kingine, hivyo basi, usiudharau wema wa Mungu kama watu wa siku za Nuhu kwa nafasi ya kuishi uliyopewa leo.

1 Petro 3:20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

 Ikiwa upo tayari leo hii kumrudia Muumba wako, unachopaswa kufanya ni kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuziacha kabisa, na kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa kuzamishwa mwili wako wote katika maji na kwa jina Yesu Kristo, kisha Bwana atakupa Roho Wake Mtakatifu atakayekuwezesha katika safari yako ya wokovu.

Matendo 2: 38 Petro akawaambia, Tubuni MKABATIZWE KILA MMOJA WENU KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

JE! TUNAMNGOJEA BWANA WAPI NA KWA NAMNA GANI?


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.


BASI ‘BWANA’ NDIYE ROHO.


UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *