WOKOVU HAUKAMILISHWI KWA TENDO MOJA HALAFU MENGINE UKAYAACHA

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Kumekuwa na mitazamo na mafundisho mengi sana ambayo yamekuwa yakiwapotosha watu wengi sana katika siku hizi za leo kuhusiana na wokovu au (kuokoka), mwingine atakuambia, ukisha tubu na kumkili Yesu Kristo kwa kinywa chako inatosha, ubatizo hauna maana tena kwasababu wapo watu wengi tu wamebatizwa lakini bado wanaendelea na maisha ya dhambi.


Mwingine atakuambia, Mungu anaangalia roho na si mwili, kwaiyo wewe vaa unavyotaka, kwa sababu wapo watu wengi tu wanaovaa mavazi ya kujisitiri lakini wanaishi maisha ya dhambi, ndugu mpendwa, usidanganyike, WOKOVU HAUKAMILISHWI KWA TENDO MOJA HALAFU MENGINE UKAYAACHA, kwani biblia inasema katika.

Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

Huwezi sema Umebatizwa katika Ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu, harafu hutaki kulitii neno, huwezi sema umetubu dhambi zako na kumwamini Yesu Kristo, harafu hutaki kwenda kubatizwa katika Ubatizo sahihi, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe, maandiko yanasema.

Yohana 3:5 Yesu akajibu, AMINAMINNAKUAMBIAMTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU.

Maana yake ni kwamba, wewe unayesema umetubu dhambi zako lakini hutaki kubatizwa kwa maji na kwa Roho huwezi uingia ufalme wa Mungu (Maandiko yapo wazi sana juu ya hilo), Hivyo, Kama hujatimiza agizo hilo, au ulibatizwa kimakosa, chukua hatua ya kurekebisha haraka sana, na Ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa mwili wako wote katika maji, na Kwa jina la Yesu Kristo, Sawasawa na maandiko.

Na wewe unayedai umebatizwa katika Ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu, na huku unapinga utakatifu (wa ndani na wa nje), jua kuwa unajidanganya, maandiko yapo wazi juu ya hilo, pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye mwona Bwana

Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFUAMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO;

Hivyo huwezi kamilisha tendo moja na kuacha moja, sharti uyakamilishe yote, tubu dhambi zako, nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi, na uishi maisha ya utakatifu, na kudumu kwa kufuata mafundisho ya mitume na manabii, na sio dhehebu lako, (vinginevyo utaishia kukataliwa siku ile).

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312

Mada zinginezo:

Je! Vazi takatifu kwa Mkristo ni kanzu kulingana na (Luka 9:3)?


MUNGU HAMDHARAU MTU YE YOTE.


MALEZI YA WATOTO (SEHEMU YA KWANZA) 


KUFANYA MATENDO MEMA HAIMAANISHI KUWA UMESHAUPATA WOKOVU

One Reply to “WOKOVU HAUKAMILISHWI KWA TENDO MOJA HALAFU MENGINE UKAYAACHA”

 • shalom
  nina tatizo yakutokukumbuka ndoto zangu lakini usiku wa leo nimeota ndoto ambozo zinanipa wasiwasi kdg
  1.mara yakwanza niliota nakula chakula
  2.mara yapili nikaota nimepewa check 6, nikaanza kununua manguo mpya, lakini baadaye kulitokea vita, ila vita vyenyewe avikuonekana ila mji mzima ulikuwa nataharuki.
  3.mara ya tatu nikaota nataka kununua samaki nikaacha.
  NIMEKUWA NIKIJIULIZA NDOTO HIZI ZINA MAANA GANI?

LEAVE A COMMENT