Kwanini safari ya wana wa Israeli kuelekea nchi yao ya ahadi (kaanani) ilikuwa imeshamiri vita?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Naomba kuuliza, kwanini safari ya wana wa Israeli kuelekea nchi yao ya ahadi (kaanani), ilikuwa imeshamiri vita na mapigano mengi mno, kwa mfano; tukisoma maandiko matakatifu baada tu ya wana wa Israeli kupita kati ya bahari, kilichofuata mbeleni kidogo yalikuwa ni mapigano na Waamaleki.

Kutoka 17:8 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.

9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.

10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. 

Na si hapo tu, mahali pengine walipigana na mfalme wa Aradi (Kutoka 21:1-4), mahali pengine walipigana na Sihoni (Hesabu 21:23-24), mahali pengine na mfalme wa bashani, mji wa Yeriko n.k. Sasa Kwanini safari hiyo ya kuelekea nchi yao ya ahadi ilishamiri vita na mapigano namna hiyo?


JIBU: Ni kweli kabisa kuwa, safari ya wana wa Israeli (mwilini), kuelekea nchi yao ya ahadi ilikuwa imeshamiri vita vingi sana njiani, na sababu ya hayo yote ni ili kutoa picha halisi kwa Waisraeli wote (ambao ni uzao wa Ibrahimu kwa njia ya imani), kuwa na wao kwenye safari yao ya kuleekea kaanani yao ambayo ni mbinguni, itakuwa si rahisi kama watu wengi wanavyodhani leo hii, bali imeshamiri vita na mapigano, shida na dhiki nyingi, kama mitume Barnaba na Paulo walivyosema.

Matendo Ya Mitume 14:21 Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, 

22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, NA YA KWAMBA IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA NJIA YA DHIKI NYINGI

Na vita yenyewe si ya damu na nyama tena, wala mapanga na mikuku, bali ni ya roho (Waefeso 6:12), hivyo jiweke tayari kwa kuvaa silaha zote roho ambazo ni.

Waefeso 6:14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 

18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Kwanini Sanduku la Mungu lilitwaliwa na Wafilisti huko shilo? (1 Samweli 4:11)


Kwanini Bwana Yesu alijeruhiwa ubavuni pale msalabani?


Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?


Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?


NAONA KUNA SINTOFAHAMU KUHUSU KRISMASI, HIVI NI KWELI IPO KWENYE MAANDIKO?

LEAVE A COMMENT