Je! Vazi takatifu kwa Mkristo ni kanzu kulingana na (Luka 9:3)?

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Luka 9:3 Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na KANZU MBILI.

Wakati Bwana Yesu alipowatuma wale mitume wake 12 (thenashara), kwenda kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu, aliwapa maagizo fulani fulani, na miongoni mwa maagizo hayo ni kuwa, mtu asiwe na KANZU MBILI, sasa je! Kanzu ndio vazi takatifu kwa wakristo kulingana na andiko hilo?  


JIBU: Kanzu linalozungumziwa hapo ni nguo ya juu, kwa lugha rahisi unaweza sema koti, (tazama picha). 

Lakini je! Vazi hilo ndio tuhitimishe kwa kusema ndio vazi pekee takatifu? Jibu ni hapana! Mavazi tunayopaswa kuvaa ni yale ambayo YANASITIRI MIILI YETU pamoja na ADABU NZURI, uwe umevaa nguo ya kijani, nyeupe, au ya blue, ilimradi tu ni ya maadili na inasitiri miili yetu haina shida, hayo ndio mavazi ambayo mtakatifu yeyote anapaswa kuyavaa, na kwa hayo, yanakua ushuhuda pia mbele za Kristo, na sio kuvalia suluali zinazobana (modo) au (model), suruali zilizochanwa chanwa, nguo zenye michoro ya ajabu ajabu, kuvalia nguo chini ya kiuno (milegezo), macheni cheni, mapete, kutoboa pua na masikio na kuvalia hereni, kusuka nywele, n.k, na zaidi ya hayo pia, mwanamume hapaswi kuvaa mavazi yampasayo mwanamke, ambapo katika siku hizi za leo shetani amewapoteza vijana wengi wa wakiume kwa kuvaa sketi kama wanawake na magauni, kwa kisingizio kuwa ni fashion, mpendwa, tambua kuwa unafanya machukizo mbele za Mungu, biblia inasema katika..

Kumbukumbu la Torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala MWANAMUME ASIVAE MAVAZI YA MWANAMKE; kwa maana KILA AFANYAYE MAMBO HAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO.

Haijalishi wewe ni nani, uwe mwigizaji, mchekeshaji (comedian), au mtu yoyote yule, ilimradi tu wewe mwanamume, unapovaa mavazi ya mwanamke wewe ni uchikizaye mbele za Muumba wako, ndivyo maandiko yanavyosema, na wote wanaochukiza sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto na kiberiti, hivyo TUBU

Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, NA WACHUKIZAO, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Usijifariji katika dhambi na ukazani kuvaa nguo za kike wakati wewe mwamume ni fashion, au kwa sababu wewe mwigizaji au mchekeshaji (comedian), basi Mungu atakusamehe siku ile, ndugu hapana! Hicho kitu hakipo, rekebisha njia zako sasa wakati ungali hai. 

Hivyo basi, kwa kuhitimisha ni kwamba, vazi lolote la maadili na lenye kusitiri miili yetu hilo ndio vazi takatifu. 

Je! Umeshampa Kristo maisha yako kwa kutubu na kubatizwa? Je! Unajua kama tunaishi katika siku za mwisho? Je! Unajua kama huna mihadi na kifo? Jiulize, kama ukifa leo hii katika hali ya dhambi bila Kristo utaenda wapi kama sio Jehanam? Hivyo mpendwa, itumie nafasi hii ya leo ukiyopewa na Mungu kwani hapendi uangamie milele.

Bwana Yesu akubariki.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Mjumbe wa agano la kwanza alikuwa ni nani?


JE! YESHURUNI NI NANI?


Omri ni nani kwenye maandiko na sheria zake ni zipi? (Mika 6:16)


Bawabu ni nani na hufanya kazi gani?


Nini maana ya mstari huu “Hatukuja na kitu duniani, na tena hatuwezi kutoka na kitu? (1 Timotheo 6:7)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *