MUNGU HAMDHARAU MTU YE YOTE.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Biblia inasema katika 

Ayubu 36:5 Tazama, Mungu ni hodari, WALA HAMDHARAU MTU YE YOTE; Ana uweza katika nguvu za fahamu. Hauhifadhi uhai wa waovu; Lakini huwapa wateswao haki yao.

Katika maisha tunayoishi huku duniani, wanadamu tumekuwa ni watu wa kumchukulia mtu kulingana na cheo chake, nafasi aliyonayo, kazi, huduma, au uchumi, lakini je! kwa Mungu wetu ipo hivyo? 


Tofauti na wengi tunavyodhani kuwa, Bwana Mungu anawatazama sana wahubiri kuliko watu wengine wote, au anawatazama sana watu wanaotoa misaada kwa wengine kuliko watu wote, au anawatazama sana masikini kuliko watu wote au matajiri sana. La! Si hivyo,  Mungu hana upendeleo kwa watu fulani tu WALA HAMDHARAU MTU YE YOTE, uwe maskini sana, uwe tajiri sana, uwe huru uwe mtumwa, Mungu hakudharau wala hana upendeleo, tena anasema mtu yoyote amchaye yeye mahali popote pale duniani hukubaliwa na Yeye.    

Matendo 10:34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;

35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.

Tunachopaswa kujua ni kwamba, Mungu hamdharau mtu na wala hajachagua watu fulani kuwa ndio bora kuliko wengine, hapana! Isipokuwa maisha yetu ya dhambi ndio yanayotufarakanisha na Mungu, lakini Yeye upendo Wake upo pale pale, (kwa nafasi iliyopo sasa hivi ya kila mtu kutubu dhambi zake na kumwamini Yesu Kristo).


Hivyo basi, ili uwe karibu na Mungu katika maisha yako na kupata kibali mbele Zake, unachopaswa kufanya ni kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako kwa kutubu dhambi zako zote na kumaanisha kuziacha kabisa, kisha nenda ukabatizwe katika ubatizo sahihi na wa kimaandiko ambao wa maji tele na kwa JINA LA YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38), na sio Kwa jina la Baba, Mwaba na Roho Mtakatifu, nawe utapata msamaha wa dhambi zako na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu atakayekuwezesha kuishi maisha ya ya utakatifu ambayo pasipo hayo hutoweza Muona Mungu (Waebrania 12:14).

Matendo 2:37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Bwana akubariki. 


Mada zinginezo:

Biblia iliandikwa na nani?


Makuhani wa Mungu ni watu gani katika biblia?


KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)


JE! UMEIAMINI INJILI IPI?


BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO 


Je! Vazi takatifu kwa Mkristo ni kanzu kulingana na (Luka 9:3)?

LEAVE A COMMENT