JE! TUNAMNGOJEA BWANA WAPI NA KWA NAMNA GANI?

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Ili tuelewe vizuri tunamngojea Bwana wapi na kwa namna gani, hebu tujifunze tu kwa mifano yakawaida katika maisha yetu ya kila siku.  

Kwa mfano; Iwapo umepatana na mtu fulani kuwa, umngoje (umsubiri), mahali fulani ili ajapo akukute hapo alipokuelekeza kusudi mpate kuonana kama mlivyokubaliana, lakini wewe kwa sababu moja au nyingine, ukaacha kukaa na kusubiri mahali hapo ambapo mtu huyo amekuelekeza, ni wazi kwamba, mtu huyo ajapo hamtaweza kuonana (mtaposhama tu), Kwa sababu haukukaa mahali husika ulipoelekezwa.

Sasa hivyo ndivyo ilivyo na kwa Bwana Wetu Yesu Kristo, wakati ule aliahidi kwa wote waliomwamini na kuwaambia kuwa, atakajua tena katika siku na saa tusiyodhani, lakini pia alitupa dalili za kuja kwake ambapo alisema 

Matayo 24:37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 

Sehemu nyingine alifananisha ujio wake na kama siku za Lutu (Luka 17:28).


Licha ya dalili hizo, pia Bwana alituelekeza mahali pa kumsubiria ili ajapo atukute hapo na ndipo mahali pekee ambapo tukikaa tutakuwa wanafunzi wake kweli kweli, na mahali hapo si pengine bali ni katika NENO lake, si katika miujiza, na wala si katika ishara na maajabu bali neno lake tu.

Yohana 8:31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, NINYI MKIKAA KATIKA NENO LANGU, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 

Mithali 8:34 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu

Na katika neno lake tunamngojea kwa kuliishi, katika kufunga na kuomba, katika mikesha na ibada, katika haki na upendo, kuvumilia dhiki na dhihaka, bila kujalisha hali zetu tulizonao sasa bali kudumu katika tumaini letu kwa Bwana huku tukiyafanya mapenzi yake kila siku, hapo ndipo tunapopaswa kunisubiri Bwana maana yu karibu.

Yakobo 5:8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, KWA MAANA KUJA KWAKE BWANA KUNAKARIBIA.

Shalom.


Mada zingineno:

BASI WAKIWAAMBIA, YUKO JANGWANI, MSITOKE; YUMO NYUMBANI, MSISADIKI. 


UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?


“Mke wa ujana wako” anayezungumziwa katika biblia ni yupi?


LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.


Tabia moja ya unafiki unayopaswa kuiepuka.


MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.

LEAVE A COMMENT