MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Tukisoma sura ya pili na mstari wa 14 wa kitabu cha maombolezo ya Yeremia, tunaona jinsi ambayo Roho Mtakatifu kwa kupitia maandiko hayo ya Maombolezo ya Yeremia, jinsi anavyoendelea kuomboleza hata sasa juu ya watu wake (kanisa) na juu ya ulimwengu mzima kwa ujumla kutokana na ubaya ule utakaoenda kuwapata wanadamu kwa kumwasi Mungu, Roho Mtakatifu bado anaomboleza juu yetu, kwa sababu maombolezo hayo, nabii wa Mungu Yeremia, hakuandika kwa mawazo yake binafsi bali aliandika akiongozwa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yake.

1 Petro 1:10 Katika habari ya wokovu huo MANABII walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa NA ROHO WA KRISTO ALIYEKUWA NDANI YAO, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 

Soma tena.

2 Petro 1:21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; BALI WANADAMU WALINENA YALIYOTOKA KWA MUNGUWAKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU

Kama nabii Yeremia alivyoomboleza juu ya Wana Ibrahimu kutokana ubaya uliowapata, ndivyo Roho Wa Kristo pia kupitia maandiko hayo hayo anavyoendelea kuomboleza sasa juu ya kanisa kutokana na ubaya utakaoenda kutupata tusipotaka kuitii injili ya kweli, Bado anasikitika na kuomboleza kutokana na mafundisho potofu ya manabii wa uongo, wanaowatabiria watu uongo na kuwafundisha uongo, wasiowaambia watu ukweli juu ya njia zao mbaya na dhambi, manabii wanaofunika uchafu wa watu na kuwafariji katika huo, wanao pinga neno la Mungu, wanahofia kuwaumiza watu hisia zao kwa kusema kweli ya maandiko, wanaojiita wa Kristo na huku wanachagua nini cha kukiamini katika maandiko (visivyo umiza hisia zao).

Maombolezo 2:14 MANABII WAKO WAMEONA MAONO KWA AJILI YAKO YA UBATILI NA UPUMBAVU WALA HAWAKUFUNUA UOVU WAKO, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa. 

Manabii wanaochanganya kweli ya Mungu na uongo, manabii yanaochanganya injili ya Kristo na hadithi za kutungwa, manabii yanaochanganya injili ya Kristo na hisia zao, manabii yanaochanganya injili ya Kristo na mawazo yao binafsi, wanao pinga ubatizo sahihi wa kimaandiko, wanao pinga utakatifu wa ndani na nje, Roho anatuombolezea kama kanisa kwa kuwa twawalizia manabii hao, kanisa linakubaliana na mafundisho yao, ambayo ndio chanzo cha sisi kukataliwa siku ile.

Matayo 7:23 NDIPO NITAWAAMBIA DHAHIRISIKUWAJUA NINYI KAMWEONDOKENI KWANGUNINYI MTENDAO

Anaomboleza Kwanini tumeacha kweli yake, Anaomboleza Kwanini tumegeukia injili nyingine (Wagalatia 1:6). Kanisa, Rejea maneno ya Bwana (maandiko Matakatifu), kwani kila adumuye katika hayo na kuyaishi atafananishwa na mtu mwenye akili.

Matayo 7: 24 Basi kila asikiaye hayo MANENO YANGUNA KUYAFANYAATAFANANISHWA NA MTU MWENYE AKILI, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 

Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zimginezo:

JE! UMEIAMINI INJILI IPI?


“HUKU WAKIDHANI UTAUWA NI NJIA YA KUPATA FAIDA” MAANA YAKE NINI? (1 TIMOTHEO 6:5)


GEUKA KATIKA NJIA YAKO NA IRUDIE NJIA YA MUNGU.


AGIZO LA MUNGU KWA WATU WOTE.


MCHUNGAJI WAKO NI NANI?


NAONA KUNA SINTOFAHAMU KUHUSU KRISMASI, HIVI NI KWELI IPO KWENYE MAANDIKO?


NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.

LEAVE A COMMENT