“HUKU WAKIDHANI UTAUWA NI NJIA YA KUPATA FAIDA” MAANA YAKE NINI? (1 TIMOTHEO 6:5)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

1 Timotheo 6:5 na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, HUKU WAKIDHANI YA KUWA UTAUWA NI NJIA YA KUPATA FAIDA

JIBU: Maneno hayo mtume Paulo alimwandikia Timotheo (na sisi pia), juu ya watu fulani, kwamba, tujiepushe na watu wa aina hiyo, watu ambao wanafikiri utauwa au kuishi maisha ya kumpendeza Mungu katika Kristo ni njia ya kupata pesa, au utajiri.

KWANINI

Kwa Sababu watu kama hao wameharibika akili zao, WAMEIKOSA KWELI NDANI YAO.

KWELI IPI?

Kweli walioikosa ni kushindwa kufahamu kuwa? Mungu hajawahi sema sehemu yoyote ile katika maandiko kwamba, kila mwanadamu duniani atakuwa tajiri au atakuwa na pesa nyingi sana, bali kinyume chake maandiko yanasema Mungu Yeye ndiye aliyewaumba MASKINI  na matajiri.

Mithali 22:2 Tajiri na MASKINI hukutana pamoja; BWANA NDIYE ALIYEWAUMBA WOTE WAWILI

TUNAPASWA KUJIEPUSHA NA AKINA NANI?

Watumishi wa injili za mafanikio. Ndugu mpendwa, Katika maandiko, Mungu hakuwahi kumtuma mtu yo yote yule ili aende kuwahubiria wanadamu jinsi kuwa matajiri au jinsi ya kutengeneza pesa,  hakuna sehemu yo yote ile, bali kinyume chake alituma watumishi wake kwenda kuwahubiria watu kuacha dhambi zao, na ndicho ambacho hata mitume walichohubiri.

Marko 6:12 Wakatoka, WAKAHUBIRI KWAMBA WATU WATUBU

Hapo mitume hawakuhubiria watu namna ya kukuza uchumi wala jinsi ya kupata utajiri, bali watubu dhambi zao. Ukiona muhubiri wa aina hiyo aisiye kwambia kuacha mizigo yako ya dhambi zako kwa kuhofia kukuchoma na kukuumiza hisia zako, basi  jiepushe nae haraka sana kwa sababu hajali kuhusu hatima ya roho yako. 


Wewe kumwamini Yesu Kristo sio tiketi ya kuwa bilionea hapa duniani (bali Mungu atakulisha kwa kadiri ya kiwango chako, kikubwa ni kudumu katika maagizo yake bila kwenda kulia wala kushoto), thawabu zako na utajiri wako unaodumu milele na milele upo ng’ambo, na sio katika dunia hii itakayoteketezwa.

Yohana 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 

Kwani umemsahau omba omba lazaro? (Luka 16:20), je! Huwakumbuki mashujaa wa imani waliotutangulia? Ambao maandiko yanasema walizunguka zunguka huko na huko wakiwa wahitaji?

Waebrania 11:37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; WALIZUNGUKA-ZUNGUKA WAKIVAA NGOZI ZA KONDOO NA NGOZI ZA MBUZIWALIKUWA WAHITAJIWAKITESWA, wakitendwa mabaya; 

38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), WALIKUWA WAKIZUNGUKA-ZUNGUKA KATIKA NYIKA NA KATIKA MILIMA na katika mapango na katika mashimo ya nchi.

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; 

Hivyo basi, mtumishi yo yote yule anayefikiri Ukristo ni njia ya kupata faida na kukuhubiria jinsi ya kutengeneza pesa jitenge nae, Mungu Hajawahi Tuma mtu kama huyo na wala maandiko hayajawahi sema Wakristo wote watakuwa mabilionea, bali imeandikwa.

Yakobo 2:5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? 

Na kuwaagiza hivi wakristo wote matajiri wanaodumu katika maagizo ya Mungu 

1 Timotheo 6:17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa UWAAGIZE WASIJIVUNEWALA WASIUTUMAINIE UTAJIRI USIO YAKINI, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.

18 WATENDE MEMAWAWE MATAJIRI KWA KUTENDA MEMAWAWE TAYARI KUTOA MALI ZAOWASHIRIKIANE NA WENGINE KWA MOYO

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni.


Kivipi tunafarakana na imani kwa kutamani fedha?


Nini maana ya mstari huu “Hatukuja na kitu duniani, na tena hatuwezi kutoka na kitu? (1 Timotheo 6:7)


TAFUTA PESA!  TAFUTA PESA! 

MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 05)

LEAVE A COMMENT