Nini maana ya mstari huu? “Na amani ya Kristo iamue miyoni mwenu” (Wakolosai 3:15)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Wakolosai 3:15 NA AMANI YA KRISTO IAMUE MIOYONI MWENU; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. 

JIBU: Tofauti na wengi wanavyodhani kuwa, andiko hilo maana yake ni ufuate kile ambacho unachokiona kipo sawa ndani ya moyo wako, au kama kuna jambo fulani basi ufuate kama moyo wako unavyokutuma, ndugu hicho kitu si sawa, hapo maandiko hayajamaanisha kuwa, kile ambacho moyo wako kinaona ni sawa ndicho ukifanye, la hasha! Biblia haijamaanisha hivyo hata kidogo kwa sababu Mungu Mwenyewe alishatuonya na kutuambia kwamba, MOYO NI MDANGANYIFU KULIKO VITU VYOTE VILE.

Yeremia 17:9 MOYO HUWA MDANGANYIFU KULIKO VITU VYOTEUNA UGONJWA WA KUFISHA; nani awezaye kuujua? 

Hivyo kamwe maandiko hayawezi kusema tuongozwe na mioyo yetu kama inavyotutuma wakati mioyo yetu ni midanganyifu kupita vitu vyote. Lakini ili tuelewe vizuri mstari huo Unamaanisha nini hapo, hebu turudie tena kusoma mstari huo kwa umakini 

Wakolosai 3:15 NA AMANI YA KRISTO IAMUE MIOYONI MWENU; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. 

Ukisoma Vizuri hapo utaona maandiko yanasema AMANI YA KRISTO NDIYO INAYOPASWA KUAMUA MIOYONI MWETU, au kwa lugha rahisi tunaweza kusema, amani ya KRISTO ndiyo inayopaswa kuitawala au kuiongoza mioyo Yetu. Sasa amani ya KRISTO ni nini?


Jibu ni kwamba, amani ya KRISTO ni MANENO YAKE ALIYOTUAMBIA, amani ya Kristo ni maneno yake tunayoyasikia kutoka kwake na yanayotufanya tuwe na amani, tumaini na saburi katika Yeye yaani kumpendeza Yeye.

Yohana 16:33 HAYO NIMEWAAMBIENI MPATE KUWA NA AMANI ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. 

Unaona hapo anaposema “HAYO NIMEWAAMBIENI” (yaani maneno yake), ili tuwe na Amani?…Ikimaanisha kuwa, maneno Yake ndiyo yanayotupa amani, maneno yake ndiyo yanayotufanya tuwe na amani katika Yeye, na maneno Yake hayo si mengine zaidi ya maandiko matakatifu (biblia). Hivyo basi, kwenye mstari huo biblia inamaanisha amani ya Kristo ambayo ni maneno yake au maandiko matakatifu, ndiyo yanayopasa kuamua, kuongoza, na kutawala mioyoni mwetu na sio tufuate hisia za mioyo yetu.


Je! Umeshatubu dhambi zako kwa kumwamini Mkuu wa uzima? Kama bado unangoja nini? Unachopaswa kufanya ni kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuziacha kabisa na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na (Matendo 2:38), nawe utapata msamaha wa dhambi zako na kupokea Roho Mtakatifu ambaye ni muhuri wake Mungu.

Waefeso 1:13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, NA KUTIWA MUHURI NA ROHO YULE WA AHADI ALIYE MTAKATIFU

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Bwana alimaanisha nini aliposema “Heri ayawe yote asiyechukizwa nami?” (Mathayo 11:6)


BWANA ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA “HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU?”


Bwana alimaanisha nini katika  (Mathayo 24:46)?


Je! Agizo la Bwana kwa mitume wake la kufufua wafu lilikuwa ni kwa baadhi ya mitume tu?


Je! Maandiko yanajichanganya katika Wakolosai 3:1 na Matendo 7:56? 


Ni maovu yapi yanayotoka kinywani mwa Bwana kulingana na (Maombolezo 3:38)

LEAVE A COMMENT