MALEZI YA WATOTO (SEHEMU YA TATU)

  Uncategorized, Watoto

FUNDISHO MAALUMU KWA MZAZI / MLEZI.

Shalom, jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe, karibu katika sehemu ya tatu ya fundisho maalumu kwa wazazi na walezi ambapo tunajifunza juu ya malezi ya watoto, na pia, kama ulipitwa na sehemu ya kwanza na ya pili ya fundisho hili, basi unaweza tembelea website ya www.Rejeabiblia.com au tuma ujumbe kwenda mamba  +255652274252 au +255 756 884 547 ili kupata sehemu hizo.


Karibu katika sehemu ya tatu.


Katika malezi ya mtoto, ni muhimu sana kumjenga zaidi kiroho tangu uchanga wake kabisa kama tulivyojifunza katika sehemu zilizopita, kwani hiyo itamsaidia kumjua Mungu na kuwa na hofu ya Mungu tangia udongo wake, lakini sambamba na hilo, yapo pia na mambo ya mwilini ambayo wewe kama mzazi wa kikristo unapaswa kumfundisha mtoto katika Malezi yake kwani yatamjenga kitabia na kimwenendo kwa kumsaidia na kujitegemea mwenyewe mahali popote pale atakapoenda kuishi, na Jambo hilo si jingine zaidi ya KUMFUNDISHA KUJISIMAMIA. 

Kama mzazi, hakikisha unamfundisha mtoto kujisimamia mwenyewe kwa kuwahi kuamka asubuhi na mapema kwa sababu kwa kufanya hivyo utakuwa umemuondolea mzizi wa kushindwa kujilisha mwenyewe baadae unaotoka na uvivu uliomo katika usingizi.

Mithali 24:33 BADO KULALA KIDOGO, KUSINZIA KIDOGO, BADO KUKUNJA MIKONO UPATE USINGIZI!

34 HIVYOUMASKINI WAKO HUJA KAMA MNYANG’ANYI, NA UHITAJI WAKO KAMA MTU MWENYE SILAHA. 

Hakikisha unamfundisha mtoto kujisimamia mwenyewe katika shughuri mabambali za nyumbani kama vile, kufagia ndani na nje ya nyumba, kuosha vyombo, kufua mavazi yake binafsi yanapochafuka.


Hakikisha unakuwa naye kalibu na kumfundisha jinsi ya kujisimamia katika shughuri za kiuchumi na uzalishaji pia, kwa mfano, mzoeshe namna ya kujisimamia katika bishara (kama wewe mzazi wa kikristo unajihusisha na hicho kitu), mzoeshe kujisimamia katika shughuri za kilimo kwa kufanya kazi za kushika jembe, n.k, mzoeshe katika shughuri za kujisimamia katika ufugaji na utunzaji wa mifugo kama kuna mifugo nyumbani.

Kama vile mfalme Daudi alivyofundishwa kujisimamia katika shughuri hizo za ufugaji wa kondoo wa baba yake..

1 Samueli 17:15 Basi Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ILI AWALISHE KONDOO ZA BABA YAKE HUKO BETHLEHEU

Ndivyo na wewe unavyopaswa kumfundisha mtoto kujisimamia pia katika shughuri mbali mbali za kimwili ili baadae awe na uwezo wa kufanya shughuri zake halali kwa mikono yake mwenyewe ili kujilisha na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada kama Injili ya Kristo inavyoagiza katika 

Waefeso 4:28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, AKITENDA KAZI ILIYO NZURI KWA MIKONO YAKE MWENYEWEAPATE KUWA NA KITU CHA KUMGAWIA MHITAJI

Na katika..

1 Wathesalonike 4: 11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, NA KUFANYA KAZI KWA MIKONO YENU WENYEWE, kama tulivyowaagiza; 

Na hapo utakuwa unamuandaa mtoto ambaye si mvuvi katika jamii na katika kazi ya Mungu, na utakuwa umeyafanya mapenzi ya BWANA MUNGU pia Ambaye Anapinga uvivu, na hivyo kutimiza wajibu wako kama mzazi wa kikristo kama ulivyoagizwa na maandiko.

Mithali 22:6 MLEE MTOTO KATIKA NJIA IMPASAYO, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Tafadhari Shea na Wazazi / Walezi wengine ujumbe huu.


Shalom.


Mada zinginezo:

MALEZI YA WATOTO (SEHEMU YA KWANZA)


MALEZI YA WATOTO (SEHEMU YA PILI). 


VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE.


Kulingana na ( 1 Petro 4:1) Ni silaha ya nia gani aliyokuwa nayo Kristo ambayo na sisi tunapaswa kujivika? 


Mbegu iharibikayo ni ipi? (1 Petro 1:23)

LEAVE A COMMENT