TEGEMEA KUPITIA GHARAMA FULANI KAMA HUKUFUATA MASHAURI NA MAONYO YA MUNGU.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Shalom, jina la Bwana na Mungu Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, Yeye ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, Aliyekuwako na Atakayekuja Mwenyezi, Amina. Karibu tujifunze neno lake (maagizo yake), ili tupate kuyashika na kuyafanya kama alivyotuagiza katika..

Walawi 22:31 KWA HIYO MTAYASHIKA MAAGIZO YANGUNA KUYAFANYA; MIMI NDIMI BWANA

Biblia inasema katika

Isaya 28:29 Hayo nayo yatoka kwa Bwana wa majeshi, MWENYE SHAURI LA AJABUAPITAYE WOTE KWA HEKIMA YAKE

Hii ikiwa na maana kuwa, Yesu Kristo Bwana wa majeshi (Zekaria 14:16), ushauri wake na maonyo yake yo yote yale ni makamilifu kabisa, hayana makosa wala mapungufu yo yote yale, kwa sababu yeye Ndiye Mshauri wa ajabu, Mwenye shauri la ajabu, na Mwenye hekima kupitia wote, na endapo mwanadamu yo yote yule akienda kinyume na maonyo na mashauri yake, basi ategemee madhara na kupitia gharama fulani tu mbeleni pindi atakapotaka kumtii Mungu, yaani hakuna namna. (hiyo ndiyo kanuni).


Sasa ili tuelewe vizuri, tunapaswa tujifunze kutoka kwa mtu wa kwanza kabisa kuumbwa ambaye ni Adamu. Siku ile Bwana Mungu (Ambaye ni Baba), alipomuumba Mtoto wake wa Kwanza (Adamu), alimpa mashauri yake na maonyo yake kwa kusema.

Mwanzo 2:16 BWANA MUNGU AKAMWAGIZA HUYO MTUAKISEMA, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. 

Lakini kama tunavyojua, baada ya Adamu na mkewe kutozingatia mashauri hayo ya Mungu na kwenda kinyume nayo, walipitia gharama fulani na madhara ambayo hadi leo hii tunayasoma katika maandiko (kwa muda wako unaweza soma kitabu cha Mwanzo sura ya tatu). Lakini sasa, kisa hicho hakikuandikwa tu kama hadithi la hasha! Bali kiliandikwa ili kutufundisha na kutuonya na sisi pia juu ya jambo hilo hilo kwamba, endapo tusipotaka kusikia na kufuata maonyo na mashauri ya Mungu, ni lazima tutapata madhara na kupitia gharama fulani tu, Kwa sababu kile alichokiagiza Mungu ndicho kilicho kikamilifu kwa asilimia zote na ndicho kilicho juu ya hekima zote na juu ya hekima ya kila kitu. Hata mfalme Sulemani ambaye maandiko yanasema alipewa hekima na akili nyingi sana na moyo mkuu kama mchanga ulioko pwani (1 Wafalme 4:29), pindi tu alipoenda kinyume na mashauri ya Bwana kwa kwenda kuoa wanawake wa kimataifa ambao Mungu aliwakataza, alipata madhara makubwa sana kwa kufanya yaliyo mabaya sana machoni pa Bwana kwa kufikia hadi hatua ya kuabudu sanamu 

1 Wafalme 11:5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. 

Na haya yote ni kwa sababu hakufuata mashauri na maonyo ya Mungu ambayo ni MAKAMILIFU YASIYO NA KASORO YO YOTE ILE.

Ndugu mpendwa, Mashauri na maonyo hayo ya Mungu hadi leo hii yapo, na si mengine zaidi ya maandiko Matakatifu, yaani neno lake, na kwamwe usitegemee kwenda kinyume na mashauri hayo harafu usipitie gharama fulani pale utakapoamua  baadae kumtii Mungu, hicho kitu hakipo, kama ulienda kinyume na maonyo na mashauri ya Mungu (biblia), tegemea kupitia gharama fulani tu katika maisha yako utakapoamua kumtii Mungu.

Wengi wetu leo hii inatulazimu kupitia gharama ya kujikana nafsi ili kusudi tuwe sawa na Mungu kwa sababu tu, watu fulani waliotutangulia waliyatupilia mbali mashauri na maonyo ya Mungu, au wale waliotushauri waliyakataa mashauri na maonyo ya Mungu tangu zamani hivyo kupelekea Bwana kusema maneno haya kwa kila anayetaka kurudi katika mastari.

Matayo 16:24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, MTU ye yote akitaka kunifuata, NA AJIKANE MWENYEWEAJITWIKE MSALABA WAKEANIFUATE

Hukusikia maonyo ya Mungu kuwa, ole wake ampaye mwengine kileo kwa kwenda kufanya biashara ya kuuza pombe na sigara, basi tegea tu kupitia gharama ya kuacha hiyo kazi yako ya kuuza pombe kama unataka kuwa sawa na Mungu.


Hukusikia maonyo ya Mungu kuwa, usiabudu sanamu, basi tegemea tu kupitia gharama ya kuukana utamaduni wako wa kuabudu sanamu, au pengine kutengwa hata na ndugu zako na kumtii Mungu, 

Hukusikia ushauri wa Mungu kuwa, Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume kwa kwenda kufanya kazi inayokulazimu kuvaa mavazi ya kiume kama vile suruali, na mavazi mengine ya kikahaba, basi tegemea tu kupitia gharama fulani kama unataka kuwa sawa na neno la Mungu. 

Na mambo mengine yote ambayo tuliyafanya kwa kuyatupilia mbali mashauri na maonyo ya Mungu, tutegemee kupitia gharama fulani kama kweli tunataka kuwa sawa na Mungu na kama kweli tunataka kuwa sehemu ya kanisa lile tukufu lisilo na doa wala kunyazi ambalo Bwana atajiletea mwenyewe siku ile 

Waefeso 5:27 apate kujiletea KANISA TUKUFULISILO NA ILA WALA KUNYANZI wala lo lote kama hayo; bali LIWE TAKATIFU LISILO NA MAWAA

Kumbuka: Ushauri wa Mungu ndio ulio bora kabisa kuliko ushauri mwengine wowote ule, Unaweza ukakuumiza hisia zako na mawazo yako lakini huo ndio ulio bora na usio na kasoro yoyote ile, Kwa sababu Mungu Ndiye Anayetupenda zaidi ya wote hapana chini ya jua. Hivyo basi, ni lazima kuyafuata mashauri yake na kabla ya kufanya Jambo lolote lile tuchunguze kama lipo sawa na mashauri ya Mungu (maandiko matakatifu), na kwa kufanya hivyo tutakuwa ni watoto wenye hekima kwa kusikiliza mahusia na maonyo ya Baba Yetu Ambaye Ni Mungu kama maandiko yanavyosema.

Mithali 13:1 MWANA MWENYE HEKIMA HUSIKILIZA MAUSIA YA BABAYEBALI MWENYE DHARAU HASIKILIZI MAONYO

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

KWANINI MNANIITA BWANA, BWANA, WALAKINI HAMYATENDI NISEMAYO?


NANYI KWA SUBIRA YENU MTAZIPONYA NAFSI ZENU


MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.


“HUKU WAKIDHANI UTAUWA NI NJIA YA KUPATA FAIDA” MAANA YAKE NINI? (1 TIMOTHEO 6:5)


“NA VITABU VIKAFUNGULIWA” NI VITABU GANI HIVYO? (Ufunuo 20:12).

LEAVE A COMMENT