MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 09)

  Siku za Mwisho, Uncategorized

Shalom, Karibu katika sehemu ya (09) ya mwendelezo wa makala yetu inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayoposha watu wengi nyakati hizi za mwisho, kama hukupata sehemu zilizopita, basi waweza tembelea website ya www.Rejeabiblia.com ili uweze kupata sehemu hizo.


Lakini awali ya yote kabisa, tunapaswa tufahamu kuwa, Maandiko matakatifu yanamuagiza kila mtu anayedai kumwamini Yesu Kristo kujichunguza mwenyewe na kujijaribu ili ajione kama kweli amekuwa katika imani ya Yesu Kristo ambayo ni moja tu (Waefeso 4:5), vinginevyo kadanganywa na anaamini imani nyingine tofauti na Ile ya kweli (haijalishi yeye ni nani).

2 Wakorinto 13:5 JIJARIBUNI WENYEWE KWAMBA MMEKUWA KATIKA IMANIJITHIBITISHENI WENYEWE. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. 

Na Imani hiyo moja na ya Kweli ni hii..Tusome.

2 Petro 1:1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale WALIOPATA IMANI MOJA NA SISI, YENYE THAMANI, katika hali ya Mungu Wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. 

Umeona hapo?..Ikiwa na maana kuwa, Imani moja na yenye thamani, ni ile waliyoipata na kuwa nayo wakina Petro, (hiyo ndiyo imani moja na ya kweli), hivyo basi, ni jukumu lako wewe binafsi (uwe nabii, mtume, mchungaji, mwalimu, askofu, Mwinjilisti, shemasi, au vyo vyote vile), kuchunguza na kuona kama Kile unachokiamini ndicho wakina Petro walichokiamini, vinginevyo umedanganywa.


Ulibatizwa ukiwa mtoto mchanga, je! Ndicho wakina Petro walichokiamini? unawaomba wafu kama vile Mtakatifu Yosefu, Paulo, Teresa n.k, wakuombee kwa Mungu, je! Hicho ndicho wakina Petro walichokiamini? Unalipigia magoti Sanamu la Mariamu, je! Hicho ndicho wakina Petro Walichokiamini? Njoo upokee nyumba na gari, njoo ufunguliwe kiuchumi, njo ununue mafuta ya upako n.k, je! Hicho ndicho wakina Petro walichokihubiri? Kama sivyo maana yake umedanganywa na unahubiriwa injili ya laana, kwa sababu huyo anahekuhubiria hayo yupo chini ya laana,

Wagalatia 1:8 LAKINI IJAPOKUWA SISI AU MALAIKA WA MBINGUNI ATAWAHUBIRI NINYI INJILI YO YOTE ISIPOKUWA HIYO TULIYOWAHUBIRINA ALAANIWE.

Hivyo jichunguze na ujirekebishe kisha urejee maandiko matakatifu (Rejea biblia yako).

Hii ni Sehemu ya tisa (09) ya makala yetu, Karibu.


JESHI LA WOKOVU (Salvation Army).

Kama tu ilivyokuwa kwa Makanisa na taasisi nyingine nyingi za uongo tulizokwisha zitazama huko nyuma, mfano Mashahidi wa Yehova, kanisa katoliki, Waadventisti wasabato n.k. Jeshi la wokovu nalo ni moja wapo ya kanisa au taasisi ya uongo inayowapotosha watu wengi katika siku hizi za mwisho kwa mafundisho yaliyokinyume na injili ya Kristo, na moja wapo ya mafundisho hayo ni kuruhusu wachungaji wanawake.

Biblia inasema katika 

1 Timotheo 2:12 Simpi mwanamke RUHUSA YA KUFUNDISHAWALA KUMTAWALA MWANAMUME, bali awe katika utulivu.

13 KWA MAANA ADAMU NDIYE ALIYEUMBWA KWANZA, na Hawa baadaye. 

Katika kanisa la kweli la Kristo, hakuna sehemu yoyote ile ambayo Mwanamke amepewa nafasi ya kumtawala mwamume kwa kuwa mchungaji wala askofu katika kanisa, na kanisa lolote lile lililo chini ya mwanamke au linaloruhusu wanawake wachungaji na maaskofu lipo kinyume na INJILI YA KRISTO likiwemo na hilo la Jeshi la wokovu pia.

Na tena injili ya Kristo inasema 

1 Wakorinto 14:34  Wanawake na wanyamaze KATIKA KANISA, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?

37 MTU AKIJIONA KUWA NI NABII AU MTU WA ROHONI, NA AYATAMBUE HAYO NINAYOWAANDIKIA, YA KWAMBA NI MAAGIZO YA BWANA.

38 LAKINI MTU AKIWA MJINGANA AWE MJINGA

Kama ukitaka kuwa mjinga wewe askofu, mchungaji, mwalimu, mtume, n.k kwa kupinga agizo hilo la Bwana, endelea tu kuwa mjinga kama biblia inavyosema. Lakini hata lini mpendwa utapenda ujinga kwa kukubali kuwa mjinga?

Mithali 1:22 ENYI WAJINGAHATA LINI MPAPENDA UJINGA? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa? 

Likini pia, katika Kanisa hilo la uongo, wapo wasioamini kabisa suala la ubatizo kitu ambacho ni kinyume na agizo la Bwana katika (Marko 16:16), lakini wale wanaoamini wanabatiza kinyume na Injili inavyosema, wakibatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, Ubatizo ambao haupo kwenye Maandiko wala hakuna Mkristo Yo yote yule aliyebatizwa hivyo, Wakristo wote katika maandiko walibatizwa kwa jina la Yesu Kristo, Mfano Wale watu Samaria (Matendo 8:16) na Kornelio.

Matendo Ya Mitume 10:48 AKAAMURU WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. 

Soma tena 

1 Wakorinto 1:13 JE! KRISTO amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? AU JE! MLIBATIZWA KWA JINA LA PAULO

Hivyo basi, kama upo chini ya watu wa taasisi hiyo ya uongo iliyo kinyume na mafundisho ya mitume, unachopaswa kufanya ni kujiepusha nao kama maandiko yanavyosema.

Warumi 16:17 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza KINYUME CHA MAFUNDISHO MLIYOJIFUNZAMKAJIEPUSHE NAO

Kumbuka: Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.


Mada zinginezo

NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.


Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)


JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?

2 thoughts on - MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 09)

LEAVE A COMMENT