Bwana alimaanisha nini aliposema “Heri ayawe yote asiyechukizwa nami?” (Mathayo 11:6)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Matayo 11:6 Naye heri AWAYE YOTE ASIYECHUKIZWA NAMI.  

JIBU: Ili tuelewe vizuri Bwana alimaanisha nini hapo, inapaswa tuelewe kwanza Yeye ni nani? Kwa sababu hapo kasema “heri awaye yote asiyechukizwa na Yeye” sasa Yeye ni nani hadi mtu achukizwe na Yeye?..Jibu tunalisoma katika..

Ufunuo 19:13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU. 

Umeona hapo? Kumbe Yesu Kristo pia ni NENO LA MUNGU, hivyo basi, hapo aliposema heri  awaye yote asiyechukizwa Nami ni sawa na kusema, heri awaye yote asiyechukizwa na NENO LA MUNGU. Mtu yoyote anayelisikia neno la Mungu na kutochukizwa nalo hata kama ni gumu na linauma kiasi, na badala yake analipokea hivyo hivyo na kuanza kulifanyia kazi kama ilivyokuwa kwa mitume, basi huyo mtu ni heri kwake.

Yohana 6:61 Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, JE! NENO HILI LINAWAKWAZA?

Soma tena

Yohana 6:65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

 66 Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.

 67 Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?

 68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 

Lakini pia, kinyume cha maneno hayo ni kweli, kwamba, mtu awaye yote atakayechukizwa na neno la Mungu pale atakapoambiwa na kutokuchukua uamuzi wowote ule wa kujirekebisha, na badala yake kuanza kubisha na kupinga kama mafarisayo, basi mtu huyu kwake itakuwa OLE na si heri tena.


Baba/Mama, unapochukizwa na neno gumu la Mungu linalochoma hisia zako kwa kukwambia mume au mke wa mtu unayeishi nae ni dhambi, basi tambua kwako NI OLE na si heri kwako, kwa sababu hukupaswa kuchukizwa nalo hilo neno bali kulipokea na kujirekebisha.


Ndugu mpendwa, unapochukizwa na neno la Mungu linalokemea uovu wako ulioufanya kwa kumtelekeza mke au mume wa ujana wako kwa sababu tu amekuwa kipofu au ni ulemavu, basi tambua kuwa kwako ni OLE kwa sababu hukupaswa kuchukizwa nalo hilo neno bali kulipokea na kujirekebisha.


Ole Mwanamke unayejiita mchungaji au askofu unapochukizwa na neno la Mungu linalokwambia hupaswi kuwa mchungaji wala askofu katika kanisa, kwa sababu hukupaswa kuchukizwa nalo hilo neno bali kulipokea, kukifanyia kazi na kujirekebisha.


Ole kijana unayesikia neno la Mungu linalokwambia kubeti ni dhambi, kutazama picha za ngono, musterbration, kunyoa viduku, kuvaa milegezo, tattoos n.k, harafu ukachukizwa na hilo neno badala ya kulipokea na kuchukua hatua za kujirekebisha kwa kutubu.


OLE Binti unayechukizwa na neno la Mungu linalokwambia kuvaa suruali, vimini, na nguo zinazochora na kuonesha maungo yako ni dhambi, Ole mwanamke unayechukizwa na neno la Mungu linalokwambia make up ni dhambi, kucha bandia, nywele bandia, kope bandia, hereni masikioni na mapini mapuani au mdomoni, kwa sababu hukupaswa kuchukizwa na hilo neno bali kulipokea na kuchukua hatua ya kujirekebisha 


Ole unayechukizwa na neno la Mungu linalokwambia kuzisujidia sanamu za Mariamu ni dhambi, kubusu sanamu unayoiita ya Yesu ni dhambi, kuwaomba watu waliokufa kama Musa, Paulo, Yasinta, Teressa n.k, kwa sababu hukupaswa kuchukizwa nalo neno hilo bali kulipokea, kulifanyia uchunguzi na kujirekebisha ili iwe heri kwako kama maandiko yanavyosema 

Luka 7:23  NAYE HERI MTU YE YOTE ASIYECHUKIZWA NAMI.

Hivyo basi, Bwana aliposema heri mtu ye yote asiyechukizwa nami alimaanisha mtu yule asiyechukizwa na neno la Mungu (neno lake)

Bwana akubariki. Shalom 

Wshirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada nyinginezo:

Bwana alimaanisha nini kusema ‘Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili?


BWANA ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA “HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU?”


Bwana alimaanisha nini katika  (Mathayo 24:46)?


Ni Mungu gani tutakayemwona na kufanana nae atakapodhihirishwa? (1 Yohana 3:2)


Kupiga panda ni nini katika  (Mathayo 6:2)

LEAVE A COMMENT