MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 10)

Siku za Mwisho, Uncategorized 2 Comments

Jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, karibu tena katika sehemu ya kumi (10) ya mwendelezo wa makala yetu inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayopotosha watu wengi nyakati hizi za mwisho.


Kama ulipitwa na sehemu zilizopita, basi unaweza tutumia ujumbe kwa namba zilizopo mwishoni mwa makala hii, ili uweze kutumiwa makala hizo zilizopita, au unaweza tembelea website ya www.rejeabiblia.com ili uweze kupata makala hizo. 

Sehemu ya kumi (10). Karibu!


KANISA HALISI LA MUNGU BABA.

Kama ilivyokuwa kwa Makanisa ya uongo na mafundisho potofu tuliyoyatazama katika sehemu zilizopita, kanisa hili halisi la Mungu Baba ni moja wapo ya makanisa hayo potofu katika nyakati hizi za mwisho yanayohubiri injili nyingine kabisa tofauti na ile iliyohubiriwa na mitume na manabii watakatifu wa Bwana, na kitu cha kuogopesha zaidi ni kwamba, Maandiko yamesha toa TAMKO la mwisho kwa kusema, “mtu yo yote yule atakayefundisha na kuhubiri tofauti na yale yaliyohubiriwa na mitume na manabii watakatifu na ALAANIWE

Wagalatia 1:8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni ATAWAHUBIRI NINYI INJILI YO YOTE ISIPOKUWA HIYO TULIYOWAHUBIRI, NA ALAANIWE

9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, MTU AWAYE YOTE AKIWAHUBIRI NINYI INJILI YO YOTE ISIPOKUWA HIYO MLIYOIPOKEA, NA ALAANIWE

Hii ni kwa wote, kwa yeye afundishaye, na wale wote wanaofundishwa na kukubaliana na upotofu huo (ambao ni wavivu wa kusoma maandiko). 

Hivyo basi, wewe unayefundisha katika kanisa hilo la uongo (Mvivu wa kusoma maandiko), na wewe unayefundishwa (Mvivu wa kusoma maandiko), wote mpo chini na ya laana, na wote WALIO LAANIWAsehemu yao ni katika moto wa milele (Bwana aliliweka hilo wazi mapema sana).

Matayo 25:41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, MLIOLAANIWAMWENDE KATIKA MOTO WA MILELE, aliowekewa tayari ibilisi na malaika zake; 

Hivyo kama upo chini ya kanisa hilo potofu   (wewe mvivu wa kusoma maandiko), paki mizigo yako na vilago vyako mapema, ili utoke huko na kujiengua katika laana hiyo, kwa kutubu dhambi zako zote na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na UDUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME, kama wanafunzi walikuwapo Yerusalemu (Matendo 2:42).

Wewe Mvivu wa kusoma maandiko, unawezaje kujiita kanisa la Mungu Baba na kumtupilia mbali Kristo? Je! Hutambui  kama kanisa la Mungu, ndio kanisa la Kristo. 

Wakolosai 1:24 Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso YA KRISTO, kwa ajili ya mwili wake, YAANIKANISA LAKE

Soma na

1 Wakorinto 15: 9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi KANISA LA MUNGU

Hivyo, huwezi kujiita kanisa la Mungu na kumtupilia mbali Kristo (umepotezwa na kudanganywa), huwezi kujiita kanisa la Mungu na kutupilia mafundisho yake kwa kuruhusu wanawake makuhani, kukana utakatifu wa nje, kuruhusu mapambo kwa wanawake, n.k, (hilo ni sinagogi la shetani), lisemalo kuwa ni wayahudi (uzao wa Israeli kwa njia ya Imani) lakini sio. Kama ilivyoandikwa.

Ufunuo 2:9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya HAO WASEMAO YA KUWA NI WAHAYUDINAO SIOBALI NI SINAGOGI LA SHETANI

Wewe Mvivu wa kusoma biblia yako, haujui kama Mungu Baba Ambaye ni Roho Ndiye Bwana Yesu huyo huyo?

2 Wakorintho 3:17 Basi BWANA NDIYE ROHO walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.

Soma tena 

Yohana 4:24 MUNGU NI ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 

Mvivu wa kusoma maandiko, hujui kama Mungu Ndiye Yesu Kristo, na Ndiye Yehova, na Ndiye Mwamba wa milele? 

Isaya 26:4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni MWAMBA WA MILELE

Au Hujui kama Mungu Ndiye Mwamba, Ndiye Roho ambaye ni Yesu Kristo?

1 Wakorinto 10: 4 Wote wakanywa kinywaji kile cha ROHO; kwa maana waliunywea MWAMBA WA ROHO uliowafuata; na MWAMBA ULE ULIKUWA NI KRISTO.

Soma tena 

Kumbukumbu La Torati 32:3 Maana nitalitangaza Jina la Bwana; Mpeni ukuu Mungu wetu. 

YEYE MWAMBA, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye Ndiye Mwenye haki na adli.

(Na hakuna miamba miwili kwenye maandiko).

Au Hujui kama Mungu Mkuu Ndiye MWOKOZI, na zaidi yake hakuna mwengine?

Isaya 43:11 Mimi, naam, mimi, ni Bwana, ZAIDI YANGU HAPANA MWOKOZI

Soma tena 

Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, Mungu mkuu NA MWOKOZI WETU

(Na hakuna waokozi wawili kwenye maandiko).

Usiwe Kama asiye na akili, aliyekosa ufahamu, Yesu Kristo Ndiye Mungu na Ndiye Baba wa milele, na Ndiye Roho, aliyeumba kila kitu ukiwemo na wewe uliyedanganywa na kiongozi wako kipofu, wavivu wa kusoma maandiko (Ayubu 33:4), na Ndiye utakayesimama mbele zake siku ile kupokea malipo yako.

2 Wakorinto 5:10 Kwa maana IMETUPASA SISI SOTE KUDHIHIRISHWA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. 

Na Ndiye atakayetawala milele na milele.

Ezekieli 20:33 Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika, NITAKUWA MFALME JUU YENU

Na ndiye aliyelinunua kanisa lake kwa damu yake ya thamani.

Matendo 20:28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha KANISA LAKE MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE. 

Hivyo basi, kanisa halisi la Mungu Baba ni kanisa halisi na mungu wa duniani hii (ibilisi) na baba wa uongo, ONDOKA HUKO NA UREJEE BIBLIA.


Kumbuka: Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 09)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 08)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 06)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)


FAHAMU NINI MAANA YA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24)

2 thoughts on - MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 10)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *