Je! Ni watu gani hao wasamao Bwana, Bwana, lakini hawatoingia katika ufalme wa mbinguni? (Mathayo 7:21)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Tukisoma biblia katika (Mathayo 7:21), tunaona Bwana alisema kuwa, si kila mtu atakayemwbia Bwana Bwana, ndiye atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Sasa swali je! Ni Watu gani hao wanaozungumziwa hapo wamwambiao Bwana “BWANA, BWANA“ lakini hawataingia katika ufalme wa mbinguni?


JIBU: Tusome kwanza andiko hilo.

Matayo 7:21 SI KILA MTU ANIAMBIAYE BWANABWANAATAKAYEINGIA KATIKA UFALME WA MBINGUNI; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 

Watu wanaozungumziwa hapo ni wale wote wanaojiita wakristo, (yaani wafuasi wa Yesu Kristo), hao ndio wanaozungumziwa hapo, kwamba, sio wote watakaoingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni wale tu watakaoyaishi na kuyafanya mapenzi ya Mungu ambayo ni maagizo yote na amri ya Bwana na Mwokozi Wetu tuliyoachiwa au kuhubiriwa na mitume wake watakatifu (injili ya Yesu Kristo).

2 Petro 3:2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, NA ILE AMRI YA BWANA NA MWOKOZI ILIYOLETWA NA MITUME WENU

Soma tena.

1 Wathesalonike 4:2 KWA KUWA MNAJUA NI MAAGIZO GANI TULIYOWAPA KWA BWANA YESU

MAANA HAYA NDIYO MAPENZI YA MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 

Ikiwa na maana kwamba, haijalishi kama wewe ni mtume au nabii, Mwinjilisti au askofu, mwalimu au mchungaji, muimba kwaya na nyimbo za injili, unamsifu Mungu kwa kuruka ruka na kumshangilia, una nena kwa lugha, unaponya wagonjwa na kutoa mapepo, unafunga na kuomba usiku kucha, unakesha hekaluni (kanisani) kama nabii mke Ana binti Fanuri, unatoa zaka na sadaka kikamilifu, lakini kama usipoyafanya mapenzi ya Mungu kwa kutii yale yaliyohubiriwa na mitume wake watakatifu, basi unafanya kazi bure, na tena, unajifurahisha katika udhalimu kwa sababu unapokataa Mafundisho ya mitume ni sawa na umemkataa Kristo Mwenyewe kama alivyowaambia mitume wake

Luka 10:16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye AWAKATAAYE NINYI ANIKATAA MIMI; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma. 

Hivyo basi, wewe kama Mkristo, hakikisha unajichunguza na kujihakiki ili kuona kama kweli unaendana na kile kilichohubiriwa na mitume na manabii (na sio dhehebu lako wala mawazo yako), na endapo ukiona upo kinyume, basi kuwa mwepesi wa kutubu kwa kuomba msamaha mbele za Mungu na kisha itii injili (kwa faida ya roho yako), kwa sababu katika siku ile utakaposimama mbele ya Muumba Wako, hautahukumiwa kulingana na hisia zako, mawazo yako, wala mtazamo wa kanisa lako, bali kulingana na injili Yake.

Warumi 2:16 katika siku ile MUNGU ATAKAPOZIHUKU SIRI ZA WANADAMUSAWASAWA NA INJILI YANGUKWA KRISTO YESU

La sivyo utaishia kukataliwa dhahiri na kuambiwa maneno haya.

Matayo 7:23 Ndipo nitawaambia dhahiri, SIKUWAJUA NINYI KAMWEONDOKENI KWANGU, ninyi mtendao maovu. 

Bwana atusaidie, Shalom.


Mada zinginezo:

NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI.


“NA VITABU VIKAFUNGULIWA” NI VITABU GANI HIVYO? (Ufunuo 20:12).


Bwana alimaanisha nini aliposema “Heri ayawe yote asiyechukizwa nami?” (Mathayo 11:6)


Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema “Kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia” Je! Alikuwa akijigamba?(Wafilipi 3:6)


KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA PILI).


TABIA NYINGINE YA IBILISI UNAYOPASWA KUIFAHAMU.

One Reply to “Je! Ni watu gani hao wasamao Bwana, Bwana, lakini hawatoingia katika ufalme wa mbinguni? (Mathayo 7:21)”

  • Kuna shuhuda moja ya mchungaji wa marekani alikufa kisha akafufuka, ”” anasema alijitahidi sana kuishi maisha ya utakatifu lakini alipokufa alikosa mbingu kwakuwa amkumsamehe ndugu yake na baada yakujikuta jehanum aliona mapepo yakitesa watu motoni nakuimba nyimbo za rihanna””
    Swali: je mapepo ndio yanayotesa watu motoni? Au je yao yenyewe ayateswi huko? Na hadhabu ya mapepo itakuwa ipi kama yao ndio yanayotesa watu? Je ushuhuda huu aupingane na neno la Mungu?

LEAVE A COMMENT