Nini maana ya mstari huu “na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorongwa vema” (Ezekieli 13:10)

SWALI: Nini maana ya mstari huu “NA MTU MMOJA AJENGAPO UKUTA, TAZAMA, WAUPAKA CHOKAA ISIYOKOROGWA VEMA” (Ezekieli 13:10)


JIBU: Tusome.

Ezekieli 13:10 Kwa sababu hiyo, kwa sababu wameshawishi watu wangu, wakisema, Amani; wala hapana amani; NA MTU MMOJA AJENGAPO UKUTATAZAMAWAUPAKA CHOKAA ISIYOKOROGWA VEMA

Mstari huo ulikuwa unaongelea tabia za manabii wa uongo wa Israeli wa wakati huo (ambao kwa sasa ni watumishi wote wa uongo, yaani maaskofu, wachungaji, wainjilisti, waalimu, manabii, mitume, n.k ), kwamba, wakati watu walipokuwa wakitenda dhambi na machukizo mbele za Mungu kwa kuasi maagizo yake, wao manabii walikuwa wakiufunika uovu wa watu hao kwa kuwaambia maneno mazuri, malaini, na kuwafariji kwamba, hakuna shida yo yote ile, kana kwamba dhambi zao na machukizo yao ni sahihi mbele za Mungu (huko ndiko kupaka chokaa isiyokorogwa vema).

Ezekieli 22:27 Wakuu wake kati yake WAMEKUWA KAMA MBWA-MWITU WAKIRARUA MAWINDOILI KUMWAGA DAMUNA KUHARIBU ROHO ZA WATUWAPATE FAIDA KWA NJIA ISIYO HALALI

28 NA MANABII WAKE WAMEWAPAKIA CHOKAA ISIYOKOROGWA VEMA, wakiona ubatili, NA KUWATABIRIA MANENO YA UONGO, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno. 

29 WATU WA NCHI WAMETUMIA UDHALIMU, wamenyang’anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki. 

Tofauti kabisa na Mungu alivyowaagiza watumishi wake manabii, kwamba, wanapaswa kuwajulisha watu dhambi zao, maovu yao, na machukizo yao na ya baba zao, ili  kusudi wapate kutubu na kumgeukia Mungu, na sio kuyaficha maovu ya mtu yo yote yule (kupaka chokaa isiyokorogwa vema)

Ezekieli 20:4 Je! Utawahukumu, mwanadamu, utawahukumu? UWAJULISHE MACHUKIZO YA BABA ZAO

Soma tena

Ezekieli 22:2 Na wewe, mwanadamu, je! Utauhukumu, utauhukumu mji huu wa damu? BASI UUJULISHE MACHUKIZO YAKE YOTE

Sasa tabia hii ya kupaka ukuta (uovu) chokaa isiyokorogwa vema, ndio inayoendelea sasa hivi katika siku hizi za mwisho kati ya manabii wa uongo, yaani waalimu wote wa uongo, wachungaji, manabii, wainjilisti, mitume, maaskofu, n.k, ambao watapaka chokaa dhambi zako za kuvaa vimini na suruali (mwanamke), mapambo bandia n.k, kwa kukwambia hakuna shida.


Watapaka chokaa dhambi zako za uasherati na uzinzi unaoufanya, mke wa mtu na mume wa mtu unayeishi nae, starehe na anasa unazozifanya, kwa kutokukukemea cho chote kile na badala yake watakutabiria baraka na kukuhubiria mafanikio. 


Watapaka chokaa isiyokorogwa vema mawazo yako mabaya na matendo yako maovu yaliyokinyume na maandiko matakatifu, na kkujufariji, kukupongeza, na kukutoa hofu kwa kukuambia Mungu ni Mungu wa upendo.


Ndugu mpendwa, Mungu ametoa onyo kai kwa watu kama hao kuwa, ataadhibu na kukomesha dhambi zote na maovu yote, pamoja na hao wanaopaka chokaa isiyokorogwa vema (yaani watumishi wa uongo).

Ezekieli 13:14 Ndivyo NITAKAVYOUBOMOA UKUTA MLIOUPAKA CHOKAA ISIYOKOROGWA VEMA, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 

15 Ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu juu ya ukuta ule, NA JUU YAO WALIOUPAKA CHOKAA ISIYOKOROGWA VEMA; nami nitawaambieni, UKUTA HUO HAUKO SASAWALA WAO WALIOUPAKA HAWAKO

16 YAANIMANABII WA ISRAELI, watabirio habari za Yerusalemu, na kuona maono ya amani katika habari zake; wala hapana amani, asema Bwana MUNGU. 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Kwanini Gombo la chuo lililokunjuliwa mbele ya nabii Ezekiel likikuwa limejaa maombolezo, na vilio na Ole ndani yake? (Ezekieli 2:10).


LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, AU ATAKAYENENA KATIKA JINA LA MIUNGU MINGINE, NABII YULE ATAKUFA.


FUNZO KATIKA HABARI YA MFALME AHABU NA NABII MIKAYA


Nini maana ya mstari huu “unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu” (2 Petro 2:21) 

LEAVE A COMMENT