JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?

Je! Utatoa hesabu ya nini katika siku ile? Utatoa hesabu ya nini katika siku ile utakayosimama mbele ya Muumba Wako? Utatoa hesabu ya nini katika ile siku ya hukumu? Kwa sababu, sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu, kama maandiko matakatifu yasemavyo.

Warumi 14: 10 Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? KWA MAANA SISI SOTE TUTASIMAMA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA MUNGU

Ili kusudi, kila mtu aweze kupokea malipo ya mambo yake yote aliyoyatenda katika mwili.

2 Wakorinto 5:10 Kwa maana IMETUPASA SISI SOTE KUDHIHIRISHWA MBELE YA KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO, ILI KILA MTU APOKEE IJARA YA MAMBO ALIYOTENDA KWA MWILIKADIRI ALIVYOTENDA, kwamba ni mema au mabaya. 

Na tena, kuamini kwako au kutokuamini kwako, hakuwezi kubatilisha hukumu ya Mwenyezi, mawazo yako na hisia zako, haviwezi batilisha hukumu ya Mungu, kama yasemavyo maandiko.

Ayubu 40:8 JE! HATA HUKUMU YANGU UTAIBATILISHA? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki? 

Kila mtu atasimama mbele Zake na kutoa hesabu ya mambo yake (bila kujali wewe ni nani), na kila mtu atakiri ya kuwa Yeye Ndiye Bwana Mungu na hakuna mwengine)

Isaya 45:22 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; MAANA MIMI NI MUNGUHAPANA MWINGINE

23 KWA NAFSI YANGU nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, YA KWAMBA MBELE ZANGU KILA GOTI LITAPIGWAKILA ULIMI UTAAPA

Sasa swali ni je! Utatoa hesabu ya nini pindi utakaposimama mbele ya Muumba wako? Je! Utatoa idadi ya chupa za bia ulizokunywa katika ulevi wako hadi kufa kwako? Je! Utatoa idadi ya pakti za sigara ulizovuta hadi kufa kwako? Je! Utatoa hesabu ya nini katika siku ya hukumu?


Je! Utatoa mbele za Muumba wako hesabu ya wanaume na wanawake uliotembea nao na kufanya nao ngono na uasherati hadi kufa kwako? Au utatoa idadi ya siku ulizolala na mke au mume wa mtu hadi kufa kwako? Je! Utatoa hesabu ya nini katika siku ya hukumu?


Mpendwa unayesoma ujumbe huu, utatoa hesabu ya nini katika siku ile? Utatoa idadi ya night clubs ulizouzulia na kufanya anasa? Utatoa idadi ya kamali ulizocheza? Utatoa idadi ya nyimbo za uzinzi na uasherati ulizoziimba? Utatoa hesabu ya nyimbo zinazofisia pombe na kuchochea mapenzi ulizoziimba? Au Utatoa idadi ya maneno machafu, uongo na matusi yaliyotoka kinywani mwako? 


Je! Utatoa hesabu ya maji na keki za upako ulizo kula na kunywa? Utatoa hesabu ya chupa za mafuta ya upako uliyotumia? Je! Utatoa hesabu ya miti na mawae (masanamu), uliyoyasujudia? Ya ng’ombe, Yesu, Tembo, Mariamu, n.k zisizo sikia wala kuona.

Zaburi 115:4 Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. 

5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, 

6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, 

7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake.

Hebu vuta picha, unasimama mbele ya Muumba wako na unatoa idadi ya mimba zisizo na hatia ulizozitoa, unasimama mbele za Mungu na kutoa hesabu ya siku ulizovaa uchi na nusu uchi kwenye luninga na mitandaoni mwanamke, unatoa hesabu ya siku ulizotembea uchi na nusu uchi barabarani, mgogo wote wazi, mapaja yote nje, maziwa yako yote na shepu ya mwili wako wote nje, na kwa kukosa akili unadhani ni urembo na ujanja kumbe ni ukahaba (Mithali 7:10) 


Ndugu mpendwa, utatoa hesabu ya nini katika siku ile? Je! Utasimama mbele za Mungu aliye hai na kutoa idadi ya wanaume wenzako uliolala nao wewe mwanaume (machukizo kwa Bwana), je! unasimama mbele za Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo na kutoa idadi ya wanawake wenzako uliolala nao kama mwanamume wewe mwanmke? (machukizo), je! Wewe mwanamke au mwanaume, utasimama mbele za Muumba Wako na kutoa idadi ya wanyama uliolala nao (uchafu na unajisi).


Utatoa hesabu ya nini wewe unayesoma ujumbe huu? Utatoa hesabu ya nini katika siku ile? Utatoa hesabu ya nini pindi utakadhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu?


Mada zinginezo:

NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI.


KUWA NA TABIA HII YA NUHU KATIKA NYAKATI HIZI ZA UOVU ILI UPATE KUSALIMIKA NA GHADHABU YA MUNGU.


Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 09)


Ni Mungu gani tutakayemwona na kufanana nae atakapodhihirishwa? (1 Yohana 3:2)

2 thoughts on - JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *