Ni maungamo gani aliyoyaungama Yesu Kristo mbele ya Pilato?


1 Timotheo 6:13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, ALIYEYAUNGAMA  MAUNGAMO MAZURI YALE MBELE YA PONTIO PILATO, 

JIBU: Maungamo aliyoyaungama Bwana Yesu Kristo siku ile mbele ya pilato, ni juu ya TUMAINI LA UFALME UJAO WENYE UZIMA WA MILELE.

Yohana 18:36 Yesu akajibu, UFALME WANGU SIO WA ULIMWENGU HUU. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 

Na sisi pia kama wanafunzi wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, hatuna budi kuyaungama maungamo hayo ya tumaini la uzima wa milele tulionao katika Yesu Kristo mbele za watu, pale tunapolaumiwa  na kushutumiwa kwa husuda kwa sababu tu!  Tunakataa uovu na kupelekwa mbele za watu, hapo hatuna budi kuweka wazi tumaini letu la uzima wa milele lililopo kwa Bwana kwa njia ya utakatifu, haki na upendo.

1 Timotheo 6:12  Piga vita vile vizuri vya imani; SHIKA UZIMA ULE WA MILELE ULIOITIWA, UKAUNGAMA MAUNGAMO MAZURI MBELE YA MASHAHIDI WENGI. 


Je! Umeshampa Bwana maisha yako? Kama bado unangoja nini? Jiulize ukifa katika hali hiyo ya dhambi utakuwa mgeni wa nani? Hivyo tubu leo dhambi zako kwa kumaanisha na kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312


Mada zunginezo:

USIMLAANI MKUU WA WATU WAKO.


ALIKUWA HAMJUI BWANA BADO, NA NENO LA BWANA LILIKUWA BADO HALIJAFUNULIWA KWAKE.


KWA SABABU NALIWAOGOPA WALE WATU, NIKATII SAUTI YAO. 


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *