Je! Tunapaswa kumuombea Shetani na Malaika zake msamaha kwa Mungu wakiwa kama adui zetu namba moja?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Je! Tunapaswa kumuombea Shetani na malaika zake msamaha kwa Mungu akiwa kama adui Yetu namba moja? Kwa sababu  ndivyo maandiko yanavyotuagiza kuwapenda adui zetu na kuwaombea wanaotuudhi (Mathayo 5:44).

Kwa Mfano: Stephano alipopingwa kwa mawe na adui zake, aliwaombea msamaha kwa Mungu juu ya dhambi ile kabla ya kufa.

Matendo Ya Mitume 7:59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. 

60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, BWANAUSIWAHESABIE DHAMBI HII. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake. 

Sasa je! Na sisi tuliomwamini Yesu Kristo tunatakiwa kumuombea ibilisi na malaika msamaha kwa Mungu?


JIBU: Jibu ni Hapana, maandiko yaliposema tuwapende adui zetu na kuwaombea wanaotuudhi, hayakumaanisha tuyapende mapepo wala Shetani na kuyaombea hayo, hapana! Bali  yalimaanisha wanadamu wenzetu kama sisi, ambapo wapo wale wanaotupenda na wanaotuudhi pia, hao ndio tunapaswa kuwapenda wote na kuwaombea bila kujali ni adui zetu au majirani zetu.

Matayo 5:43 Mmesikia kwamba imenenwa, UMPENDE JIRANI YAKONA UMCHUKIE ADUI YAKO

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 

Na wala si ibilisi na malaika zake (mapepo au malaika walioasi).


Sasa ni Kwanini hatupaswi kuwaombea msamaha kwa Mungu Ibilisi na malaika zake ili wasamehewe na kurudishwa tena mbinguni?

Jibu ni kwamba, Ibilisi na malaika zake hawawezi samehewa tena, kwa sababu maandiko yanasema, nafasi zao, au sehemu zao, au mahali pao, HAPAKUONEKANA TENA MBINGUNI baada ya kuasi,

Ufunuo 12:7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 Nao hawakushinda, WALA MAHALI PAO HAPAKUONEKANA TENA MBINGUNI

Maana yake ni kuwa, Shetani na malaika zake hawana tena sehemu yo yote ile mbinguni bali ni kwenye moto wa milele baada ya hukumu (Matayo 25:41)


Hii ni kutufundisha nini?

Hii ni kutufundisha kuwa, Mungu Huyu Mwenye huruma na upendo, fadhiri na rehema zisizo na kikomo, anao pia upande wa pili wa safaru.

Warumi 11:22 Tazama, basi, wema na UKALI WA MUNGUKWA WALE WALIOANGUKAUKALI, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; KAMA SIVYOWEWE NAWE UTAKATILIWA MBALI

Ndio maana wale wote waliopata neema hii ya wokovu kwa kuitii injili ya Mungu iliyohubiriwa na mitume na manabii Wake watakatifu, tunaagizwa kuufanyia kazi wokovu wetu, au neema hii tuliyoipata kwa KUOGOPA NA KUTETEMEKA.

Wafilipi 2:12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA

Kwa sababu Mungu anao upande wa pili wa sarafu.

Yuda 1: 5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, AKIISHA KUWAOKOA WATU KATIKA NCHI YA MISRIALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI

6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. 

Hii inatisha na kuogopesha mno, Hivyo kimbilia kwa Mungu siku zote kwa kupiga magoti na kujinyenyekeza kama mtoto mdogo, kwa sababu sisi si kitu hata kidogo mbele Zake.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

KWANINI BIBLIA INAMFANANISHA IBILISI NA SIMBA ANGURUMAYE?


Kwanini Kuzimu kuongeze tamaa yake na kufunua kinywa chake bila kiasi? (Isaya 5:14).


Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?


Kwanini safari ya wana wa Israeli kuelekea nchi yao ya ahadi (kaanani) ilikuwa imeshamiri vita?


Kwanini Sanduku la Mungu lilitwaliwa na Wafilisti huko shilo? (1 Samweli 4:11)

LEAVE A COMMENT