JINSI LAANA YA ROHO MTAKATIFU INAVYOENDELEA MIONGONI MWA WAHUBIRI WA INJILI PASIPO KUJIJUA.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Ipo laana ya Roho Mtakatifu inayoendelea miongoni mwa wahubiri wa injili pasipo hata wao wenyewe kutambua, na laana hii ya Roho Mtakatifu inaanza tu pale ambapo muhubiri anapohubiri injili nyingine yo yote iliyo kinyume na ile iliyohubiriwa na mitume na manabii.

Haijalishi wewe ni nani, una sifa gani, una wadhifa gani, una mali nyingi kiasi gani au ni fukara kiasi gani, pale tu unapohubiri kitu kingine tofauti na kile kilichohubiriwa na mitume na manabii watakatifu, basi unalaaniwa.

Wagalatia 1:8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni ATAWAHUBIRI NINYI INJILI YO YOTEISIPOKUWA HIYO TULIYOWAHUBIRI, NA ALAANIWE

9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, MTU AWAYE YOTE AKIWAHUBIRI NINYI INJILI YO YOTE ISIPO KUWA HIYO MLIYOIPOKEA, NA ALAANIWE

Sasa unaweza uliza, ni kwa namna gani ni laana ya Roho wakati mtume Paulo ndiye aliyetamka maneno hayo? Jibu ni kwamba, hayo sio maneno ya mtume Paulo bali ni ya Roho, kwa sababu Kristo (alipokuwa katika mwili), aliwaambia mitume wake kuwa, yo yote mtakayoyasema si Ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu ndani yenu (Mathayo 10:20), maana yake kile kilichohubiriwa na mitume ni cha Roho Mwenyewe aliyekuwa ndani yao. 

Hivyo, laana hii ipo juu yako wewe muhubiri wa Injili unapohubiri kinyume na kile kilichohubiriwa tayari (Ndivyo Roho alivyosema kwa kupitia mtume Paulo).

Wagalatia 1:9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, MTU AWAYE YOTE AKIWAHUBIRI NINYI INJILI YO YOTE ISIPO KUWA HIYO MLIYOIPOKEA, NA ALAANIWE

Laana hii ya Roho ipo juu yako wewe muhubiri unayehubiri kuwa hakuna moto wa milele, laana hii ipo juu yako wewe unayehubiri kuwa, kuna mitume wanawake kwenye maandiko, Mungu ameruhusu wanawake kuwa mitume, Mungu ameruhusu wanawake kuwa wachungaji, Mungu ameruhusu wanawake kuwa maaskofu, (kitu ambacho ni kinyume kabisa na injili ya Kristo inavyosema askofu awe MUME wa mke mmoja na sio mke wa mume mmoja)

1 Timotheo 3:2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, MUME WA MKE MMOJA, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; 

Laana hii ya Roho pasipo kujua ipo juu yako wewe muhubiri wa injili unayehubiri na kutufundisha Kuwaomba wakina Mariamu, Petro, Paulo, ambao ni wafu (lakini katika Kristo (Ufunuo 14:13), kwamba watuombee kwa Mungu, kitu ambacho Kristo wala mitume wake hawakukihubiri, na tena maandiko yanasema awaombaye wafu anafanya machukizo mbele za Mungu, na tena, Petro wala Paulo, wala Yakobo wala Musa, hawakusema wala kuhubiri TUWAOMBE wao baada ya kufa kwao ILI WATUOMBEE kwa Mungu, bali walisema tuombe kwa Baba, ambaye ni Mungu, ambaye ni Bwana, aliye Roho).

2 Wakorinto 3:18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao KWA BWANA, ALIYE ROHO. 

Ambaye ni BWANA NA MWOKOZI (Yesu Kristo), na zaidi yake hapana mwokozi mwengine

Isaya 43:11 Mimi, naam, MIMI, NI BWANA, ZAIDI YANGU MIMI HAPANA MWOKOZI

Mungu Mkuu, Mungu wa kweli na uzima wa milele, ambaye kila goti litapigwa mbele zake (Isaya 45:23).


Laana hii ipo juu yako wewe muhubiri unayesema ubatizo wa maji sio jambo la lazima, kutawadhana miguu haina maana, kushiriki meza ya Bwana haina haja (ilikuwa ni ishara tu), kufunika kichwa kwa Mwanamke wa kikristo asalipo sio lazima.


Laana hii ipo juu yako wewe unayehubiri na kusema, Mungu ameagiza tumwabudu siku ya jumamosi (Sabato), kitu ambacho ni kinyume na maandiko kwa sababu biblia inasema tumwabudu Mungu kwa haki na utakatifu SIKU ZETU ZOTE.

Luka 1:74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, NA KUMWABUDU PASIPO HOFU

75 Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake SIKU ZETU ZOTE

Laana hiyo ipo juu yako wewe muhubiri wa aina hiyo kwa sababu Roho kwa kupitia Paulo alisema 

Wakolosai 2:16  Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au MWANDAMO WA MWEZIAU SABATO

17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. 

Hivyo jiondoe kutoka katika laana hiyo ya Roho mapema, kwa kutubu na kuigeukia Injili ya Kristo, na kudumu katika mafundisho ya mitume (Rejea maandiko matakatifu na udumu katika hayo).

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

BASI ‘BWANA’ NDIYE ROHO.


FUNZO KATIKA HABARI YA MFALME AHABU NA NABII MIKAYA


Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?


Kwanini Kuzimu kuongeze tamaa yake na kufunua kinywa chake bila kiasi? (Isaya 5:14).


Je! Agizo la Bwana kwa mitume wake la kufufua wafu lilikuwa ni kwa baadhi ya mitume tu?


KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA PILI).

LEAVE A COMMENT