Maana ya mshipi wa dhahabu matitini ni ipi (ufunuo 1:13)

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU,Tusome…

Ufunuo 1:13 “na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa MSHIPI WA DHAHABU MATITINI”.

Tafsiri ya moja kwa moja ya Neno mshipi ni mkanda,soma Mathayo 3:4, na Matendo 21:11, na Zaburi 18:32, utaliona jambo hilo, pia mkanda huo unaweza ukawa umetengenezwa kwa namna yoyote ya malighafi, pengine kwa ngozi au kitambaa kigumu,kwa ujumla ni lazima ibane sehemu ya kiuno au kwenye kifua..

Yule Mtume Yohana aliyemwona kwenye maono si mwanamke kama wengi walivyofikiri,hapana bali ni Mwanaume ambaye ndiye Yesu Kristo..

Ukiendelea kusoma mbele anajitambulisha kwa kusema…

Ufunuo wa Yohana 1:17-18[17]Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

[18]na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu

.

Na Kama tunavyofahamu mwenye uwezo wa kuzichukua hizi funguo na mwenye uwezo nazo na aliyekuwa amekufa na sasa yu hai, hakuna mwingine zaidi ya Bwana Yesu, hivyo inatuonyesha alikuwa ni Bwan mwenyewe..

Kwanini alivikwa mshipi matitini na sio kifuani?

Hiyo ni kutuonyesha au kutupa picha kwamba ni sehemu gani ya mshipi huo uliweza kufungwa, ambayo (matitini ni sehemu ya mwili wa mwanamke) na pia haimlengi Bwana kama ana matiti,hapana, au kumtaja Bwana kama mwanakondoo haimaanishi kwamba anasura kama kondoo,bali ni lugha ambayo inaujumbe wake rohoni..

Mathayo 3:4 “Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na MSHIPI WA NGOZI kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu”.

Hata sisi hatuna budi kujifunga mshipi viunoni mwetu, na mshipi wetu tunaoufunga ni KWELI YA NENO LA MUNGU

Waefeso 6:13-14[13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

[14]Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani..

Utakatifu ndilo vazi letu linalotufunika juu mpaka chini,(Ufunuo 19:8), na tunapojifunga KWELI YA NENO LA MUNGU KATIKA VIUNO VYA ROHO ZETU, tunakuwa Katika ukamilifu na kuwa safi mbele za Mungu..

Umejifunga Neno la Mungu?

Neno la Mungu linasema…

1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake”.

Bwana anazidi kusema..

Mathayo 22:37 “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote”.

Ikiwa bado wewe ni rafiki wa dunia basi fahamu kabisa neno la Mungu hujalifunga kama mshipi kiunoni na upo kwenye hatari kubwa ya kukumbana na ghababu ya Mungu siku ya mwisho, jifunge neno la Mungu leo ili uweze kishinda kila uovu Katika zama hizi za giza…

Maran atha..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *