MACHUKIZO NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Machukizo ni nini?

Machukizo linatokana na neno chukizo,  ni hali inayokupelekea kujawa na hasira au chuki ndani yako, ndo mana kwa Mungu,kitu chochote kinachomfanya aipandishe ghadhabu yake,kitu hicho kinaitwa chukizo”

Vitu vifuatavyo vinamtia Mungu Machukizo

1. Ibada ya Sanamu.

Mfano wa kitu chochote chenye muundo wa sanamu kilikuwa ni machukizo makubwa kwa Mungu, ndicho kisababishi cha kwanza chenye kumtia Mungu wivu

Kumbukumbu 27:15 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina”.

Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.

17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa”.

Soma pia Kumbukumbu 27:15, na 2Wafalme 23:24

2. Uasherati na ulawiti.

Walawi 18: 22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”.

Soma tena Mambo ya Walawi 20:13

3. Mavazi yasiyopasa.

Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”

Kuvaa mavazi yasiyokupasa kwa Jinsia yako ni machukizo kwa Mungu, Mwanamke kuvaa suruali za kiume na mwanaume kuvaa magauni ya mwanamke ni machukizo na aibu pia..

4. Sadaka yenye kasoro.

Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.

Kumbukumbu 17:1 “Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.

Lakini pia lipo chukizo moja KUU na KUBWA ambalo litatokea kule YERUSALEMU, ambalo ni CHUKIZO LA UHARIBIFU, linalomhusu Mpinga-kristo.

Kwa Maelezo zaidi kuhusu chukizo hilo tutafute kwa namba zetu hapo chini..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *