FURAHA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Furaha ni hisia chanya ambayo mtu anakuwa nayo pale ambapo anakuwa amefanikisha mambo fulani kwa wakati alioutarajia au asioutarajia ni matokeo ambayo humfanya mtu kuridhishwa na yale au hali alionayo kimaisha .

Kibiblia furaha ni moja wapo ya tunda la roho Mtakatifu ambapo mtu anapokuwa amepata kipawa cha roho Mtakatifu moja kwa moja mtu huyu anakuwa na furaha ya wokovu ambayo inamfanya wakati wote awe mwenye furaha katika kumtumikia Mungu.. Pia ni furaha ambayo inadumu katika hali zote na nyakati zote njema na ngumu .

Katika maandiko tunaweza kuona Mfano wale mamajusi walipoona tena ile nyota ya Bwana kule Bethelehemu, walifurahi.

Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno”.

Pia utaona hata wale waliokwenda kaburini kwa Bwana Yesu,Na kukuta ameshafufuka, Biblia inasema walifurahi sana.

Mathayo 28:8 “Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari”.

Vivyo hivyo hata malaika mbinguni wanapoona mtu mmoja ametubu dhambi, huwa wanafurahi pia.

Luka 15:10 “Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”.

Hivyo furaha huwa inatokana na kupatikana kwa jambo fulani lililokuwa lina tarajiwa kukamilishwa ndani ya muda fulani…


TUNAWEZAJE KUIPATA FURAHA YA KIMUNGU

Hii Ni furaha ambayo huwa inazidi furaha zote yaani ni furaha ambayo haina mipaka hata katika nyakati za shida furaha huwa ipo, kifupi ni furaha ambayo huwezi kuielezea jinsi inavyopatikana kama furaha nyingine zinavyopatikana…Ni aina ya furaha ambayo haiathiriwi na hali au mazingira…
Furaha hii inaletwa na Bwana wetu YESU KRISTO mwenyewe.
Nifuraha inayoletwa baada ya mtu kwa kumaanisha mwenyewe kwa kinywa chake kumpokea Bwana wetu YESU KRISTO kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Mungu anakuwa na jukumu la kummiminia furaha hii kwa Roho Mtakatifu atakayempokea kipindi hicho.


Warumi 15:13 “Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu”.


1Nyakati 16:27 “Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake”.


Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.Luka 2:10 “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;


11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”.


Yokobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”


1Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.


Kwa muda wako pitia vifungu hivi
1Petro 1:8, Yohana 17:13


Na wewe pia ukiwa ni mmojawapo wa wanaohitaji kupokea furaha hii ya ki- Mungu katika maisha yako ambayo si watu wote wanaweza kuipokea utakuwa umefanya uamuzi wa busara sana…Kwa sababu ni Yesu pekee ndiye anatoa Furaha hii na wala hakuna mwingine…


Maandiko yanasema hivi:


Zaburi 5: 11 “Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia”.


Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.


Unaona? Basi fungua leo moyo wako, Kristo aingie ndani yako, kukusamehe, na kukuwekea furaha idumuyo.. Ikiwa Upo tayari leo kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, basi wasiliana nasi kwa namba chini ya somo hili…


Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *