WAKILI NI NANI KIBIBLIA?

Maswali ya Biblia No Comments

Wakili kibiblia ni mtu aliyepewa jukumu la kusimamia nyumba, au kaya ya mtu mwingine, na hii inajumuisha usimamizi wa kifamilia na si hapo tu huenda hadi katika mali alizo nazo Bwana wake.
Jambo hili tunaweza kuliona katika kitabu cha
mwanzo15:2, pale ambapo Eliezeri alipokuwa wakili wa Ibrahimu kwa kuwa mwangalizi wa mali za Ibrahimu

tusome
Mwanzo 15:2
2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?

Na si huyo tu, tunaona pia yusufu naye alikuwa wakili wa mali za Potifa akida wa farao

Mwanzo 39:2-6

2 Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.
3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.
4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.

Na katika agano jipya, tanaona tena, Bwana Yesu analizungumzia jambo hili la Uwakili, na hapa haswa aliakuwa anawazungumza watumishi wake wanaofanya kazi ya kulichunga kundi, wanapaswa waweje
tusome

Luka 12:40-48
40 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
41 Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia?
42 Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
43 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.
44 Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
45 Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;
46 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.
47 Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.

Ni jambo gani Bwana alitaka kujifunze hapa, ikiwa wewe umepewa Uwakili, au umefanywa kuwa wakili wa kusimamia kundi la Bwana,  kuwaongoza watu katika Imani, lazima uwe mwaminifu katika jambo hilo ambalo Bwana amekuweka, yaani jukumu lako kuu au dhamana uliyopewa ya kulisha kundi la Bwana unapaswa   ulifanye Kwa uaminifu Kwa kuwahubiria iliyo kweli pasipo kupindisha jambo lolote , ndiyo maana (ukisoma mstari wa 47) anasema “mtumwa anayejua mapenzi ya Bwana wake na asiyatende atapigwa sana” fanya Kwa uwaminifu Uwakili wako. Hapo ni kuwa makini katika kulitunza kundi alilokupa Bwana.

Pia jambo hili halikuwa Kwa watumishi tu, Bali na  kwa waaminio, Wewe ambaye umemwamini Yesu Kristo katika maisha yako na kila siku unaenda kanisani, wewe pia ni wakili wa Bwana, kwa kupitia karama aliyokupa Mungu au huduma yoyote, iwe kuimba, kufanya usafi kanisani, kuongoza kundi fulani katika idara mfano wamama, wababa, vijana nk., kufuta viti vya kanisa, kupangusa vumbi, kukirimu, kupatanisha nk..
haya yote Bwana amekupa ili uyasimamie, na uyatimize pasipo ulegevu bali katika biidii tena pasipo kusukumwa wala kulazimishwa, maandiko yanasema heri mtumwa yule ambaye Bwana wake atakamkuta anafanya hivyo Kwa uaminifu, hivyo tumia vyema huduma yako na karama yako katika kumwakilisha Bwana Vyema katika maisha yako

1Wakorintho 4:1  Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.2  Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

Ikiwa bado ujaokoka, basi Leo mwamini Yesu Kristo ili Kile alicho kupa kipawa na karama  ukiwakilishe vyema

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *