MAKURUHI NI NINI?

  Maswali ya Biblia

Makuruhi ni neno lenye  maana ya “kuchukiza kulikopitiliza” ,ni kama kumkosea mtu sana.., mfano tuseme mabeberu ni makuruhi kwa watu wa Africa, akimaanisha mabeberu ni watu wanaochukiza sana africa, watu wa africa hawawapendi kabisa mabeberu, kwasababu ukiangalia Katika historia ni watu waliowatesa sana na kuwaonea na kufikia hatua ya kuwafanya watumwa…

Neno hili tunalipata hapa,

1 Samweli 13:4-5

[4]Waisraeli wote wakasikia habari ya kwamba Sauli ameipiga hiyo ngome ya Wafilisti, na ya kwamba Waisraeli wamepata kuwa makuruhi kwa Wafilisti. Basi hao watu wakakusanyika pamoja kumfuata Sauli huko Gilgali.

[5]Nao Wafilisti wakakusanyana ili wapigane na Waisraeli, magari thelathini elfu, na wapanda farasi sita elfu, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.

Habari hiyo tunaona ni baada ya Israel kuvamia kambi za wafilisti na kuwapiga, hivyo Israel kwa kuona wameshinda na kuanza kujigamba,ndipo wafilisti wakaeka chuki na Israel,na kulazimika kwenda kukusanya jeshi kubwa kama mchanga wa bahari ili kupigana na Israel, hiyo yote ni kwasababu Israel ilifanyika makuruhi kwa wafilisti..

Lakini  habari kamili tunaijua,jinsi Mungu alivyowashindia watu wake Israel…..

Jambo hili tunaona limejirudia, ni vita kati ya Palestina (Wafilisti) na Israel, Imefika sehemu Palestina imeweka chuki kubwa jambo ambalo tunajua kabisa ni mpango wa Mungu ili Maaandiko yatimie lakini pia ni kwa ajili ya Mungu kujichukulia utukufu kwa vita vitakavyopiganwa siku za Karibuni pale Israel  ( Soma Ezekieli 38 &39).

Na Israel haijawa makuruhi tu kwa Palestina ,hapana, bali itafika kipindi mpaka dunia nzima Ili kutimiza unabii wa vita ile kuu ya Har Magedoni ambayo itapiganwa pale Israeli, siku za mwisho. Vita hiyo itakuwa kati ya Israeli na mataifa yote duniani..

Zekaria 12:3 “Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake”..

Unapoyafahamu hayo ndugu na pengine kuyaona kabisa, usione ni ishara nzuri kwako wewe ambaye ujampokea Kristo ndani ya maisha yako.. siku si nyingi mambo hayo yanakwenda kuwa wazi, na hapo unyakuo utakuwa umeshapita, Jiulize utakuwa wapi wewe?

Tubu leo kwa kumaanisha kabisa,Ukabatizwe upokee Roho Mtakatifu akuongoze kwenda Mbinguni..

1Wathesalonike 5:3 “Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT