PENTEKOSTE NI NINI?

  Maswali ya Biblia

JIBU..

 Pentekoste ni Neno la kigiriki lenye maana YA HAMSINI, ilikuwa ni desturi ya wayahudi kusheherekea siku ya hamisini baada ya pasaka na waliagizwa na Mungu wewe wanafanya hivyo, ijapokuwa kwao walikuwa hawaiiti Pentekoste bali waiita ni SIKU KUU YA MAJUMA…

Na hii ilitokea baada ya Mungu kuwaambia wahesabu majuma 7 ,yani sabato 7 kila baada ya pasaka, yani siku ya 49 na siku ya hamsini ndiyo Pentekoste iwe sikukuu,Soma (Kumbu. 16:9 na Walawi 23:15).

Kwasababu mambo hayo yaliyofanyika agano la kale ni kivuli cha agano jipya, kulikuwa na ulazima mkubwa wa sikukuu hizi kuwa na uhusiano na agano letu hili jipya, ndo mana pasipo kutazamia wakashangaa Roho Mtakatifu anashuka juu yao siku ya Pentekoste ambayo kwao walikuwa wanasheherekea sikukuu ya majuma ,jambo ambalo hawakuwahi kulifikiri, ni kama vile kusulubiwa kwa Bwana Yesu kulivoangukia Katika siku yao ya Pasaka..ndivyo hata kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kuliangukia Katika sikukuu  yao ya Majuma

Je na wewe umemwagiwa Roho Mtakatifu,Umempokea Yesu Kristo moyoni mwako, Kumbuka Roho Mtakatifu ni halisi na ni bure kumpata, tazama anabisha rohoni mwako…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT