Mwandamo wa mwezi ni nini ki-Biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!.

Mwandamo wa mwezi(mwezi mpya) kijiografia katika kipindi hiki mwezi unakuwa katikati ya Dunia na Jua. Nusu ya mwezi inakuwa haipati mwanga wa jua.

Sasa katika Agano la Kale mwezi mpya unapoanza yaani siku ya kwanza ya mwezi kwa Wayahudi ilikuwa ni siku Takatifu ambayo Bwana aliagiza hivyo kwa wana wa Israeli na kuna mambo ambayo Mungu aliwaagiza wayafanye wana wa Israeli katika siku hiyo ya kwanza ya mwezi.( yaani tarehe 1 ya mwezi mpya “siku ya kwanza”).

Mambo ambayo ilikuwa lazima wayafanye wana wa Israeli katika kipindi hicho ama inapofika siku hiyo. Ilikuwa ni lazima watoe sadaka za kuteketezwa, kupiga tarumbeta pamoja na sadaka mbalimbali kama vile sadaka za Vinywaji. Ukisoma HESABU 28:11-15 utaliona jambo hilo na pia katika siku hiyo haikuruhusiwa mtu yeyote kufanya kazi yoyote ama biashara ya namna yoyote. Soma pia NEHEMIA 10:31-33 utaliona jambo hilo pia.

Hesabu 28:11 “Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;

12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za

unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja;”

Mungu aliagiza wafanye hivyo kila mwandamo wa mwezi. Tusome pia.

Hesabu 10:10 “Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu”.

Walikuwa wakifanya hivi siku zote kwa uaminifu kabisa Wayahudi lakini ilikifikia wakati wakawa wanafanya kwa mazoea tu(kutimiza ratiba tu). Jambo hili lilimchukiza Mungu ikapelekea Mungu kuzikataa sikukuu hizo.

Isaya 1:13 “Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.

14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua”.

Maana walikuwa wanafanya sikukuu hizo huku mioyo yao ikiwa mbali na Mungu huku wamejaa uovu nk.

Je! Jambo hili linaendelea mpaka sasa/Ni sahihi kuendelea kufanya hivyo katika agano jipya?.

Hapana!, katika agano jipya hatupaswi Tena kufanya hivi kama vile sheria ya kwenda kwa kuhani na mbuzi ama kondoo kwa ajili ya dhambi kufunikwa ama kama vile tusivyoitunza tena katika agano jipya Sheria ya kuishika sabato maana tunajua Sabato ni Bwana wetu Yesu Kristo. Hivyo hivyo pia katika Mwandamo wa mwezi pia.

Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo”.

Maana sasa hatuko chini ya sheria yaani torati.

Je!, ni kipi tunachojifunza juu ya haya maagizo ambayo Mungu aliwapa wana wa Israeli?

Bwana anatufundisha pia kudhamini siku inapoanza na inapoisha, kuthamini wiki inapoanza na inapoisha, kuthamini mwaka unapoanza nq unapoisha na mwaka vile vile.

Inapoanza siku,wiki,mwezi au mwaka ni wakati mzuri wa kutafakari tumeongeza nini katika kuujenga ufalme wa Mbinguni!? Pia kukutanika na wengine (ndugu katika Kristo kumfanyia Mungu ibada).

Mungu akusaidiee kila tunapoanza siku tuitamini kwake na tumshukuru kwa Neema yake

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya mfundisho ya NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1<< 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *