Wasamaria ni watu gani katika Biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Bwana Yesu asifiwe.

Wasamaria kama tunavyosoma katika Biblia hawa walikuwa ni watu kutoka samaria kaskazini Mwa mji wa Yerusalemu. Baada ya ya Israeli wote kupelekwa Ashuru utumwani nchi ya Israeli ilibakia tupu bila mtu yoyote.

Mfalme wa Ashuru wa Ashuru aliwachukua watu wengine(Wasamaria/wageni) ili kwenda kuikalia nchi ile ili isiwe poli.

Sasa hawa wasamaria hawakuwa wakimuabudu Mungu wa Israeli bali walikuwa wakiabudu miungu yao. Yaani walikuwa ni wapagani.

Baada ya kuishi kipindi kifupi Maandiko yanatuambia walitokea wanyama wakali kama simba wakaanza kuwauwa hao wageni(Wasamaria).

Na hiyo ilitokea ni kwasababu Wasamaria walienda na miungu yao katika taifa la Israeli pasipo kufahamu nchi hiyo ni Takatifu na hakukutakiwa kuwa na miungu yoyote inayoabudiwa ila Mungu wa Israeli tu.

Baada ya Mfalme wa Ashuru kupata taarifa alimtuma kuhani mmoja myahudi. Ili kwenda kuwafundisha kanuni na taratibu za kuishi katika hiyo nchi ambazo kanuni hizo walitakiwa kuzifata za Mungu wa Israeli na sio za miungu yao waliyokuja nayo.

Kuhani alienda na vitabu vya torati na Wasamaria walikubali(kuviamini ) vitabu vitano na kimoja cha Yoshua vingine vyote vilivyosalia hawakuvikubali yaani kiviamini hawakutumia.

Hiyo ikafanya wazishike Sheria za Mungu lakini hawakuzishika zote wakawa pia wanaabudu miungu yao wanachanganya na Mungu wa Israeli pia.

Na hii hata baadae Israeli walipoachiwa kutoka utumwani wakalejea katika nchi yao wakawakuta wasamaria na hawakutaka kuchangamana nao maana waliwaona kuwa ni wapagani.

2 Wafalme 17:24
“Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake.

25 Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao.

26 Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika MIJI YA SAMARIA, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi.

27 Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi.

28 Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha BWANA.

29 Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa.

30 Watu wa Babeli wakafanya Sukoth-benothi kuwa mungu wao, watu wa Kutha wakafanya Nergali, watu wa Hamathi wakafanya Ashima,

31 Waavi wakafanya Nibhazi na Tartaki; nao Wasefarvi wakawaunguza wana wao katika moto kwa Adrameleki na Anameleki, miungu ya Sefarvaimu.

32 Basi hivyo wakamcha BWANA, nao wakijifanyia wengine wao kuwa makuhani wa mahali pa juu, ambao waliwafanyia dhabihu katika nyumba za mahali pa juu.33 WAKAMCHA BWANA, NA KUITUMIKIA miungu YAO WENYEWE, sawasawa na kawaida za mataifa ambao wao walihamishwa kutoka kwao.

34 Hata siku hii ya leo hufanya sawasawa na kawaida za kwanza; wala hawamwogopi BWANA, wala hawazifuati sheria zao, wala hukumu zao, wala ile torati, wala ile amri BWANA aliyowaamuru wana wa Yakobo, ambaye alimpa jina la Israeli”

Ukisoma mstari wa 33 utana kweli walikuwa wanamcha Bwana na kuitumikia miungu yao jambo ambalo lilikuja kufanya Israeli wasitake kabisa kuchangamana nao hata kidogo.

Lakini alipokuja Bwana Yesu ndio akapata kuiondoa hiyo tofauti maana wasamaria walikuwa na mahali pa kuabudia katika Mlima Gerizimu na huko walijenga hekalu walilokuwa wakimuabudu Bwana Israeli wakaona ni hekalu la kipagani.

Pia wayahudi nao walikuwa na mahali pa kuabudia katika Hekalu lile la Sulemani (Mlima moria) bali Yesu alisema “Wamwabuduo Bwana watamwabudu katika roho na kweli”  hivyo si myahudi kwenda Yerusalemu wala msamaria kwenda mlima Gerizimu bali ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli.

Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, AMBAYO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”

Je!, na wewe unamwabudu Mungu katika roho na kweli? Yaani katika Roho Mtakatifu na kutembea katika Neno lake Bwana wetu Kristo Yesu?.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya mfundisho ya NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *