NENO I.N.R.I LINAMAANISHA NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno hili I.N.R.I ni maneno ambayo katika baadhi ya picha nyingi za Bwana Yesu ambapo alikuwa msalaba, limeonekana neno hili, lakini ukisoma katika maandiko neno hilo huwezi kuliona

Tusome

Yohana 19

19 Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.

20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani.

ukisoma hapo katika sura ya 19, pilato alitoa agizo, kwamba pale juu ya msalaba alipo Bwana Yesu kiweke kibao ambacho kiliandikwa maneno, ambayo yaliandikwa Kwa lugha tatu, ili Kila atakaye pita asome, lugha hizo zilikuwa ni kiebrani, kiyunani na kirumi

Na maneno yenyewe yalikuwa
YESU MNAZARETI, MFALME. WA WAYAHUDI
Sasa maneno haya kwa lugha ya kirumi au kilatino yalisomeka hivi

Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum.” Na kifupi chake ndio hiyo I.N.R.I…

Lakini Ukweli ni kwamba juu ya msalaba, hayakuandikwa maneno yale katika ufupisho wowote, bali yaliandikwa vile vile kama yalivyokuwa tena kwa lugha zote tatu, ili kila mtu aliyepita aweze kuyasoma, na ndio maana wale Mafarisayo wakamwambia Pilato. Usiandike, kuwa huyu ni Mfalme wa Wayahudi; bali andika kuwa yeye ndio anajiita, mfalme wa Wayahudi…Unaona ikiashiria kwamba maandishi yale yalikuwa yanasomeka kabisa na sio kwamba yameandikwa kwa kifupisho fulani.

Lakini pamoja na hayo yote, kujua au kutokuja msalaba ulikuwaje, kwamba ulikuwa ni mrefu sana, au ni mfupi sana, au ulikuwa ni wa alama ya kujumlisha, au ni wa nguzo iliyosimama, au kwamba maandishi yake yaliandikwa kwa wino wa bluu au wa njano, Hayo yote hayachangii chochote katika wokovu wetu?? Kwasababu hata katika Neno hilo hilo YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI, ukisoma injili nyingine utaona linasema tu MFALME WA WAYAHUDI(Marko 15:26), na sehemu nyingine linasema HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI(Luka 23:38)..Unaona sasa ukiyatafsiri hayo katika lugha ya kilatino (kirumi) utaona ni tofauti kabisa na hiyo yenye kifupisho cha INRI.

Na madhehebu mengi baadhi hususani, Katoliki, Anglikana na Lutheran, wanapenda kutumia Ufipisho huo wa lugha ya kilatino (kirumi), kiyawakilisha yale maneno yaliyoandikwa juu ya msalaba wa Yesu.

Sasa hii imepelekea watu kuuabudu msalaba sana, zaidi kuliko kufikiri kazi ya msalaba ni nini haswa , hivyo hayo yasikuchanganye, sana sana tazama JE MSALABA WA BWANA WANGU YESU UMEKOMBOA MAISHA YANGU
Je kupitia msalaba nimepata ondoleo la dhambi zangu. Ukiyafahamu hayo itakuwa Bora zaidi..
Basi ikiwa bado ujampa Yesu Kristo maisha yako huu ndiyo wakati alikufa Kwa ajili yako YESU ANAKUPENDA MPOKEE LEO

UBARIKIWE
Kwa Maombezi/Ushauri/Maswali/Ratiba za Ibada. Wasiliana nasi Kwa namba hizi
+225789001312/ +225693036618

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya mafundisho ya NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10<< 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *