Ni Makao ya aina gani Yesu alikwenda kutuandalia (Yohana 14:1-3).

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kabla ya kujua ni makao gani Bwana wetu Yesu Kristo ni vizuri kwanza tukajua kwa picha ya kawaida nini maana ya Makao?

Makao ni Sehemu au Mahali anapopachagua mtu ampabo hapo ataendesha maisha yake ama kufanya shughuli nyingine kwa kadili apendavyo ama atakavyo yeye.

Lakini kwa mtu yeyote asiekuwa na makao maalumu yaani yeye hana sehemu maalumu ya kutulia na kuendesha huenda shughuli zake ama kupumzika utaona huyo mtu cha kwanza hana utulivu, anakuwa hajulikani sehemu gani anapatikana anakuwa ni mtu wa kutanga tanga utaona leo yuko huku kesho kule kesho kutwa yuko sehemu nyingine tena. Maisha yake yanakuwa ni ya kutanga tanga tu.

Sasa liko jambo la kujifunza tunapokwenda sasa kuona jambo ambalo Mungu alilifanya!,

Mungu alipoamua kumuumba Mwanadamu alikuwa ni roho tu wala hakuwa na mwili sasa alipokusudia mwanadamu aliemuumba aishi hapa duniani ndio akapata wazo la kumuumbia mwili ambao utakuwa ni nyumba au makao ya roho!. Sasa huo mwili ndio unaomsaidia Mwanadamu kuishi na kufanya shughuli zinazoshikika na kuonekana katika ulimwengu/dunia hii. Huo mwili ndio unaomsaidia kupumzika,kuishi na kupumzisha roho yake akiwa hapa duniani.

Sasa Bwana Yesu alisema anakwenda kutuandalia makao kama tunavyosoma….

Yohana 14 :1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.

Sasa kwa kawaida roho zote huwa hazina miili kama tuliyonayo sisi. Hivyo huwa zinatanga tanga tu hazina makazi maalumu sasa zinachofanya ni kuwaimgia wanadamu ambao hawa maji ya uzima ndani yao yaani ambao hawajamuamini Yesu Kristo. Sasa zikishafanikiwa ndio zinapata mahali pa kupumzika na roho Zaidi ya 20 zinaweza kuweka makao ndani ya mwili wa Mwanadamu!.

Maana zinapokuwa huko nje zinatanga tanga zinakuwa hazina raha yoyote!.

Ndio maana Bwana Yesu alisema….

Mathayo 12:43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”.

Hivyo Mwanadamu ana makazi(makao) ya aina mbili ambayo ndio yanayomsaidia  yeye kuishi hapa duniani na kuona raha ya kuishi.

Makao ya kwanza ni mwili wake amabao pia maandiko yanasema (Ni hekalu la Roho Mtakatifu ambamo pia Roho wa Mungu anakaa ndani yake pale mtu anapomuamini Bwana Yesu).

Na makao ya pili ni Nyumba inayofanywa kwa mikono ya wanadamu yaani nyumba hizi tunazoishi mimi na wewe.

Hivyo tutakapoondoka hapa duniani tukifika kule mbinguni tutakuwa na makao bora kuliko yote ya aina mbili. Makao ya kwanza ni ile miili mipya isiyoharibika ambayo mimi na wewe tuliomwamini Yesu atakapokuja hata ile siku ya unyakuo tutakuwa na hiyo miili mipya ya kimbinguni ambayo haizeeki,haipati magonjwa,haisikii njaa, nk Haleluya tufanye hima maana ipo kwa ajili yetu Bwana kawaandalia wampendao mimi na wewe.

Ndio maana Mtume Paulo anasemaa….

2 Wakorintho 5 :1 “Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.

2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;

3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.

4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima:

Na makao/makazi ya pili ni majumba ambayo tukifika huko tutayakuta yaliyobora zaidi kuliko haya tuliyayo huku yaliyofanywa kwa mikono ya Mwanadamu.

Ukiendelea kusoma anaendelea kusema

1Wakorintho 5:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda”

Hivyo tumeandaliwa mambo mazuri sana na mwokozi wetu ambayo maandiko yanasema jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi kusikia haleluya!! Atukuzwe saba Mungu wetu!!

Ubarikiwe sana.

Maranatha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *