Tofauti  iliyopo kati ya ndoto na maono ni ipi?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Ndoto Ni mtiririko wa wa picha na mawazo pamoja na hisia zinazokuja wakati mtu akiwa hajitambui yaani amelala!, na zinakuja wakati asioujua yeye, anapopata usingizi tu basi mfululizo wa picha na mawazo vinaanza kujitengeneza vyenyewe tu.

Na pia mtu anakuwa hapangi nini aote leo au asiote kabisa!, hii inatokea tu kwa kila mtu awe tayari au asiwe tayari ataota tu ndoto hivyo unapoota ndoto hakuhitaji utayari wako kabisa.

Na ndoto kwa sehemu kubwa sana ndoto anazoziota Mwanadamu zinatokakana na shughuli za kawaida kabisa anazokuwa anazifanya

Muhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;………. ”

Lakini pia ndoto zimegawanyika katika makundi matatu!, ndoto za Ki-Mungu(Mwanzo 28:12),  ndoto za Shetani na shughuli za kawaida.

Je! Maono ni nini sasa?.

Maono yanatofauti kidogo sana na ndoto!, ijapokuwa Maono hayatofautiani sana na ndoto.

Maono maono ni mfululizo/mtiririko wa picha  na hisia yanayokuja wakati mtu akiwa hajalala akiwa na akili zake timamu na anajitambua kabisa. Pia kama ilivyokuwa kwenye ndoto tulivyoona kuwa mtu hapangi aote nini anapokuwa amelala, vivyo hivyo kama katika maono mtu hapangi nini aone!!.

Yaani mtu mwenyewe haamui kuwa ni aina gani ya maono anayotaka aone ila ni ghafla tu anapokuwa amekaa ama anatembea au anasoma neno,ama anajifunza anaona vitu vya tofauti tofauti na mazingira halisia aliyopo.

Huenda akawa eneo fulani na akaona kitu fulani katika eneo hilo ambacho kwa uhalisia kabisa hakipo kwa wakati huo.

Sasa anapotoka katika hiyo hali yeye mwenyewe kabisa anaona alikuwa hajalala hata.

Pia hivyo hivyo maono yapo yanayotokana na shughuli za kawaida, maono yanayotoka kwa Mungu na yale yanayotoka kwa yule mwovu.

Na maono yanawatokea watu wengi sana wenye depression (Msongo wa mawazo) watu wanaotumia madawa ya kulevya nk. Na Shetani mara nyingi anawaletea maono wanajikuta wanaona mambo ya ajabu ajabu tu!.

Lakini wapo watu wengi pia wanaodhania kila alieokoka ni lazima aone maono kutoka kwa Mungu!, jambo hili si kweli maana suala la kuona maono au kutabili ama kuponya, nk hivyo ni vipawa vya Roho Mtakatifu na si vya mtu tu kwamba anajipangia awe na nini hapana! Na ni jambo lisilowezekana kila mtu akawa na vipawa vyote hayupo huyo mtu. Ila Yesu Mwokozi peke yake. Soma 1 Wakorintho 12:29-31.

Hivyo jumla ya yote maono na ndoto sio kipimo ama neema ya kipekee sana la!, Neema ya kipekee ni kuzaliwa mara ya pili katika Kristo Yesu na kuliishi Neno la Mungu.

Maono na ndoto sio kipimo cha utakatifu, kipimo cha utakatifu ni kuongozwa na Roho!!!

Ubarikiwe sana.

Maranatha!!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *