Je tumaini ni nini , na ninani basi tunapaswa kumtumainia ?

  Maswali ya Biblia

Tumaini ni hali Fulani ya nafsi/ akili yenye kutarajia matokea mema/chanya juu ya jambo fulani kuja kutokea .
Katika kumtumikia Mungu sisi kama wateule wa Kristo Tumaini ni moja ya nguzo muhimu katika Ukristo katika nguzo tatu ambayo ya kwanza ikiwa ni UPENDO, Ya pili ni IMANI na ya tatu ni Tumaini. (1Wakorintho 13:13).
Hivyo hivi viwili vya mwisho vinatabia ya kwenda pamoja sambamba , pia biblia inatumbia Imani ni kuwa na uhakika wa mambo YATARAJIWAYO, ni bayana ya mambo yasiyoonekana…(Waebrania 11:1)ikimaanisha kuwa ilituwe Na Imani lazima tumaini la imani yetu liwepo ndani yetu kwa kile ambacho tunakitarajia kutokea.

Lakini kimaandiko tumaini ni tarajio, au tazamio juu ya mambo fulani ambayo unatiazamia tayari kuwa yatakuja . Tofauti na tafsiri za kawaida tunazozifahamu ya kwamba tumaini ni tarajio la jambo ambalo pengine unaweza ukawa hata huna uhakika nalo, kwamfano, Waathirika wa virusi vya ukimwi upo ushauri nasaha ambao wanapokea Yakwamba wanapaswa kuishi kwa matumaini . Hivyo kuupelekea kukubaliana na hiyo hali ya udhaifu huku wakiwa na matumaini ya kuishi kwa muda mrefu.

Lakini katika ukristo ni tofauti kidogo huwa hatusemi kuwa tukifa tunatumainia kwenda mbinguni kana kwamba hatuna uhakika wa jambo hilo au hatusemi tunatumaini tunatumainia tukifa tutakwenda mbinguni, la hasha au hatusemi tunatumaini Bwana Yesu atakuja kwa imani uwakika huo tunao kabisa. Na ndio maana ya Imani na ndio katika kuamini hilo ndipo ambapo tumaini linazaliwa ndani , hivyo katika kuamini huko ndipo tumaini halisi linaweza kuzaliwa huko hapo ndipo twaweza kusema tunatumainia moja ya siku hizi tutamwona Bwana Yesu akitokea mawinguni… Hapo sasa tumaini la imani lije ,isipokuwa tunatazamia atakuja katika siku hizi za usoni na hata kama asipokuja leo wala kesho basi ni sawa lakini mwisho wa yote ni lazima aje tu…

Hivyo ni muhimu kwa kila mkristo kuwa na kiwango kikubwa cha Tumaini ndani yake, katika safari hii ngumu na ya majaribu mengi hapa duniani ni muhimu TUMAINI liumbike ndani yetu kwamba siku si nyingi Bwana wetu atatuokoa…Na ndio maana tunaimba..’’Ni salama rohoni mwangu, Bwana Himiza siku ya kuja,’’ ..tunatumaii kuwa siku moja hayo yote yatakwisha, tunapopitia misiba ya ndugu zetu tunatumaini siku moja tutawaona tena utukufuni uso kwa uso, na na mambo kama hayo yanatupa nguvu ya kuweza kusonga mbele bila kukatata tamaa.hivyo , tunapopitia mateso, dhiki na njaa na kuchukiwa na kutengwa, na kudharauliwa tunajua ni kwa kitambo kidogo tu tunatumaini siku moja isiyokuwa na jina Bwana Yesu atatufuta machozi na mambo kama hayo hayatakuwako tena …Hilo ndilo tumaini hasaa linalotoka katika uhakika Fulani…ambao bado hatujaufikia maadamu tupo hapa duniani.

Bila kuwa na tumaini, katika safari hii ya wokovu kamwe hatuwezi kufika mbali kama vile tu, bila Imani na Upendo, hakuna chochote tunachoweza kufanya.Kwasababu tumaini linavutwa na subira na uvumilivu.

Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.

3 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;

4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;

5 na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.Biblia inaendelea kusema…
Wagalatia 5:

5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.

Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena TUNAMTAZAMIA Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

Inasema tena…
2Petro 3:13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, MNATAZAMIA mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. 14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.

Hivyo kwa kumalizia tumaini ni matarajio au matazamio ya ahadi tulizoahidiwa, Lakini Imani ni uhakika wa matarajio hayo. Au twaweza kusema kuwa ni uhakika wa tumaini letu.

Bwana akubariki.

Shalo

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT