Maana ya Marko 4:11 KWA WALE WALIO NJE YOTE HUFANYWA KWA MIFANO.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Yapo mambo mengi sana ambayo Mwokozi wetu Yesu Kristo aliyazungumza ama kuyafundisha kwa mifano iliyo dhahiri kabisa lakini ndani ya mifano humo kulikuwa na Mafumbo ambayo si kila mtu aliyaelewa wapo watu wachache sana waliomuelewa kwa ile mifano aliyozungumza iliyokuwa na mafumbo yanayolenga jambo fulani!!?

Sasa unaweza kujiuliza kama Yesu alikuja kutuokoa hapa duniani sisi wanadamu ni kwa nini tena atumie mifano tena yenye mafumbo na anaelewa kabisa atakapozungumza watu hawatamuelewa? Ni maswali mengi sana unaweza ukajiuliza yeye alietuletea wokovu iweje tena aseme mafumbo tusielewe na mambo mengine mengi.

Lakini huenda hatufahamu jambo muhimu sana juu ya Yesu Kristo Mwokozi wetu na wokovu wake kwa ujumla! Ni kweli kabisa Lengo au kusudi la Mungu ni watu wote wapate ondoleo la dhambi na wageuke waziache njia zao.

Lakini kitu usichokifahamu ni kwamba Neema ya Kristo ama wokovu wake na kuzijua siri za ufalme wa Mbinguni haya mambo yanahitaji watu waliotayari na waliodhamiria kweli kweli.

Yaani ni kwamba “Neema ya Kristo inafanya kwazi na watu wanaoitaka” vile vile mafumbo aliyokuwa anayasema Bwana Yesu “wanaotaka kufahamu na kutembea katika mapenzi ya Mungu ndio wanaofumbuliwa mafumbo hayo na kufahamu wasio taka kamwe watabaki kujua mafumbo tu basi.

Sasa ni kwa namna gani? Si kila aliekuwa akimfuata Yesu alikuwa anataka kujifunza na kuelewa na kuokoka la!, Kuna wengine walikuwa wanafata miujiza tu basi hakuwa na haja na fundisho!, wengine walikuwa wanataka kuponywa tu basi, wengine walikuwa wanamfuata kwa ajiri ya kumpeleleza wapata namna ya kumstaki, Kuna wengine walio kuwa na nia kwelii ya kukaa katika fundisho na kumuelewa Mungu, wengine walikuwa wanamfuata tu kwa ajili ya kusikiliza Maneno yake yenye hekima, wengine walikuwa wakimfuata kwa sababu tu yeye ni maarufu nk.

Na ndio maana utaona mifano ambayo alikuwa akiitoa katikati ya watu zaidi ya elfu tano 5000 waliokuwa wanamfuata faragha ni ni watu wasiozidi 100. Hebu fikiria zaidi ya watu hao wanaomfuata na kumuuliza ni idadi isiyofika hata robo.

Sasa maandiko yanasema…..

Marko 4:10 “Naye alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza habari za ile mifano.

11 Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, BALI KWA WALE WALIO NJE YOTE HUFANYWA KWA MIFANO,

12 ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa”

Unaona hapo anasema “……BALI KWA WALE WALIO NJE YOTE HUFANYWA KWA MIFANO,”

Maana yake kumbe si machache la!, ni mengi tunaweza kusema yote wao kwao walitoka na mifano tu!!

Yesu hakuwa anatishwa na wingi wa watu ndio aanze kuwaambia siri wazi wazi LA!, Bwana wetu hakuwa hivyo kabisa. Havitiwi na wingi wa watu na hawako tayari bali anavutiwa na uchache wa watu walio tayari walio maanisha kweli kweli, 

Lakini leo hii utaona kila siku watu wanakwenda kanisani Lakin bado ni wazinzi,walevi,watukanaji, wenye hasira nk hawana badiliko ama ushuhuda wowote katika maisha yao ya wokovu watu kama hawa kamwe kwao itakuwa ni kwa mifano tu wala hawatatambua kabisa. Wamekaa kanisani miaka mingi wanashiriki meza ya Bwana wanafanya kila kitu.

Lakini leo hii ukiwaambia Kuna utawala wa miaka 1000 hawajui,unyakuo hawajuii ndio kwanza ni jambo jipya, hawajui mambo mengi juu hata kanisa tulilopo ni la Mwisho ambalo sifa yake imetajwa kwenye kitabu cha UFUNUO wa Yohana.

Ni wakati wakuamua kujitwika msalaba wako na kuwa moto kweli kweli usiwe vuguvugu Bwana kasema atakutapika.

Kumfuata Yesu Kuna gharama mtu asikudanganye, gharama yenyewe ni kujitwika msalaba wake mwenyewe!!

Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake”?

Hivyo na sisi tumaanisha tusiwe kama wale makutano maana zama hizi ni za Mwisho unyakuo upo karibu sana.  Tengeneza taa yako weka na mafuta ya ziada kama wale wanpawali watano walitwa na mafuta ya ziada wakimgojea Bwana arusi.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *