Nini Maana ya Bisi katika Biblia? Walawi 23:14.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Bisi zinazotajwa katika maandiko yaani Biblia ni tofauti kidogo na Bisi tunazozifahamu sisi.

Tunafahamu Bisi tunazozijua sisi katika taifa letu ni yale Mahindi ya njano mdogo madogo maarufu yanajulikana kama “Mahindi ya bisi” ambayo hukaangwa na kisha hufutuka/kulipuka lipuka kisha yanabadilika rangi kuwa Meupe kwa Lugha ya kigeni huitwa
PARCHED” lugha iliyozoweleka kwa watu wengi ni POPCORN.

Sasa kwa watu walioko mashariki ya kati yaani Israeli, Syria, nk bisi zao ni tofauti na sisi, ambapo sisi tunakaanga mahindi lakini wao  kule Bisi zao ni ngano, pia wanazikaanga  vile vile kama sisi tunavyokaanga mahindi. Na tofauti yake muonekano wake haubadiliki sana kama jinsi ulivyo wa mahidi yanavyobadilika.

Walawi 23:14 “Nanyi msile mkate, wala BISI, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote”.

Vifungu hivi vingi viko vingi sana vinazungumziwa katika Biblia hasa katika agano lile la Kale utaona hata Mungu anawapa maagizo wana Wa Israeli Wasile kitu chochote katika vile wanavyovivuna ikiwemo bisi,Masuke, mpaka watakapokileta miguuni mwa Bwana kile kinachomstahili yeye.

Yoshua 5:10 “Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko.

11 Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na BISI, siku iyo hiyo”.

Vipo vifungu vingi utaviona lakini hapa tutaviorodhesha vichache.

Soma pia….

1Samweli 17:17 “Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako;

18 ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao.

Tunalisoma Neno hilo tena….

1Samweli 25:18 “Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.

19 Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.

Je! Tunajifunza nini katika Neno hili?, au ni kipi Mungu anachotufundisha sisi katika Agano hili jipya?.

Jambo tunalojifunza hapa kama wana wa Mungu ni kwamba!, katika vile vyote Mungu anavyotubariki tusifikirie kula tu kwanz ama kufanya mambo yetu tu kwanza la!, tuhakikishe kwanza Fungu la Mungu tunalitenga Pembeni na kulitoaz kisha Sasa vinavyobakia basi tuvitumie kwa mahitaji yetu ambayo tunahitaji kama ni mavazi,wazazi, familia,  na jamaa wengine wote wa Karibu na jamii nzima kwa ujumla ikiwa iko ndani ya uwezo wako.

Hivyo Mungu ndio atakavyozidi kutubariki zaidi pale tunapomuweka kuwa wa kwanza kabla ya kufanya jambo lingine lolote!.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *