Elewa tafsiri ya Mithali 29:25, kumwogopa mwanadamu huleta mtego.

  Maswali ya Biblia

Mithali 29:25
[25]Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;
Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

JIBU..

Ukiendelea kusoma anasema…

Mithali 29:25b

Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama

Unapokuwa na hofu yoyote kuhusiana na wanadamu watakuonaje unapoamua kufanya jambo lolote la KiMungu fahamu utajikuta Katika upotevu mkubwa sana..hofu ya wazazi wako watakuonaje unapoamua kuokoka na kumfata Kristo, hofu ya watu watakuonaje unapoamua kuvaa mavazi ya adabu na Heshima,unaona utaitwa mshamba, hofu zote za kutaka kuwapendeza na kuwafurahisha wanadamu wenzako hazina utukufu wowote mbele za Mungu…

Ndo mana tunamwona mfalme sauli alipoteza uthamani wake kwa Mungu kwa kutaka kuwapendeza wanadamu kwa kumwacha agagi hai 1samweli 15:25

Tunamwona haruni pia ilikuwa bado kidogo tu aangukie kwenye mauti baada ya kuwapendeza wana wa Israeli kwa kuwaundia ndama ya sanamu Kutoka 32:22-24

Tunaliona pia kwa herode kumkata kichwa Yohana mbatizaji ili ampemdeze Mwanae na mke wake Marko 6:21-27..

Mtawala mwingine herode alipomuua mtume Yakobo na kutaka kumfunga Petro gerezani,yote kwasababu alitaka Wayahudi wampende,awapendeze Matendo 12:1-4

Mwisho wa hawa wote waliishia Katika mitego ya wanadamu na hofu nyingi, kwamba wasipotenda kwao wataonekanaje,maisha yao yalijaa wasiwasi na mashaka

Lakini Katika yote ni kwamba wanaomtumaini Bwana siku zote lazima watakuwa salama,

Watumishi wa Mungu,Shadraka, Meshaki, Abnego walipoikataa amri ya Mfalme ya kuabudu sanamu, wakaazimia kumtii Mungu, ijapokuwa walitupwa Katika tanuru la moto lakini hawakuteketea,walitoka salama..

Daniel kwa Ile hofu ya Mungu iliyokuwa ndani yake ilimfanya hata kutupwa Katika tundu la simba aliona si chochote, lakini sikuzote wanaomtumaini Bwana wanakuwa salama kama alivyotoka akiwa mzima…

Maandiko yanasema..

Yohana 5:44

[44]Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?

Hatuna budi na sisi tuifate ile njia Yesu Kristo aliyotuchagulia,hakuna namna,ili tuwe salama kwa Bwana, haijalishi uone dunia imekuacha nyuma kiasi gani,au imekutenga , njia ni moja ya kujikana nafsi ili tuzidi kuwa salama…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT