Elewa maana ya Mithali 18:9 “Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu”.

Maswali ya Biblia No Comments

SWALI: Je, huu mstari una maana gani?

Mithali 18:9 “Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu”.

Mharabu maana yake ni mharibifu.. hapo inaonyesha jinsi gani uvivu unavyoweza kuleta uharibifu katika mambo au vitu na kuonyesha jinsi uvivu na uharibifu vilivyosambamba.

Mfano mtu anayefanya Kazi ya Ujenzi wa ghorofa chini ya ubora, kwasababu ya kutokuwa makini na Kazi yake atajenga ghorofa bovu na kupoteza pesa nyingi alizopewa kwaajili ya Kazi hiyo lakini pia na kuhatarisha maisha ya watu, siku likianguka watu wengi watapoteza maisha. Huyu hana tofauti na mharibifu.

Watu wengi wamepata matatizo ya kiafya kwasababu ya kula vyakula vilivyoandaliwa chini ya ubora. Mtu ambaye ni mvivu hutafuta njia ya mkato Ili kufanikiwa na hii kupelekea madhara kwa wengine

Vilevile katika Kazi ya Mungu wengi waonapo mambo waliyotarajia kupata yanachelewa au kupatikana kwake ni vigumu, hubuni njia za mkato na kutunga mafundisho ya uongo na kutumia njia zisizo ruhusiwa na Mungu lengo lao wawapate wengi kiharaka.
Tunashindwa kusubiri, kwa kujifunza na kuomba kwa mda mrefu, badala yake tunayaruka madarasa ya Mungu, tunasoma njia ya jangwani inachosha,wala haina faida,hatupati chochote na kuifata njia ya kora….. Matokeo yake Kazi ya Mungu tunaifanya chini ya ubora, tunawapoteza wengi, kwa elimu na injili ya uongo.

Maandiko yametuonya sana katika kuifanya Kazi ya Mungu yanasema.

Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu..”

Tuitwapo kumtumikia Mungu katika nafasi yoyote ile iwe uchungaji,ushemasi, uimbaji, utume nk.tukubali na gharama. Kwani “tumeaminiwa uwakili ” kama alivyosema mtume Paulo, tukijua ifikapo siku ya hukumu tutatoa hesabu ya utumishi wetu (1Wakorintho 9:16-17). Hivyo yatupasa tuwe makini mno, tusije kuwa waharibifu kwasababu ya uvivu wetu.

Bwana atusaidie

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *