Nini maana ya donda ndugu?

  Maswali ya Biblia

2 Timotheo 2:16-17
[16]Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,


[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

Neno donda ndugu, ni kidonda kinachoweza kutokea kwenye sehemu ya mwili,baada ya damu kushindwa kupita kwenye kiungo kimojawapo, Katika vidole au viungo vya ndani ya mwili na mwishowe ndiko hutengeneza kidonda kisichoweza kupona..

Na ikiwa kiungo hicho kisipoweza kuondolewa Katika mwili basi kidonda hicho husambaa mwili mzima na kuleta madhara makubwa zaidi,ni kama kansa jinsi ilivyo,na jawabu la mwisho ni kupata tiba au kukiondoa kiungo hicho

Kuna wakati mtume Paulo aliyafananisha Mafundisho ya uongo ya Himenayo na Fileto kama ugonjwa wa donda ndugu ulivyo..

FILETO na HIMENAYO walifundisha kwa watu yakuwa kiyama ya wafu ilishapita, hakuna kiyama huko mbeleni, hakuna kitu kinaitwa unyakuo huko mbeleni, unyakuo umeshapita..

Na yote kwasababu Mafundisho hayo ni hatari,yasipokataliwa na kupingwa vikali yanaweza kusambaa kwa watu na kuleta mvurigikano katika Imani za watu na kupelekea kupoa si hata kufa kiroho..

Ukishawawekea watu imani kwamba hakuna tena unyakuo, Wala Bwana harudi tena maana yake unawafanya waendelee kudumu kwenye dhambi na kuendelea kujiita wakristo,kwa kuwa ndani yao hakuna tumaini lolote la maisha ya mbeleni..

Kuna wakati mtume Paulo alilionya kanisa lililokuwa thesalonike.. tusome

2 Wathesalonike 2:1-6

[1]Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,

[2]kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

[3]Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

[4]yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

[5]Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

[6]Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati

wake.

Kulingana na Biblia takatifu,unyakuo bado haujatokea lakini wakati wowote kanisa la kweli la Mungu litaondolewa pamoja na watakatifu walioukataa ulimwengu na kujiepusha na mambo maovu na kujitakasa kwa Neno la Mungu watanyakuliwa na Bwana Katika utukufu wake, lakini kitakachokuwa kimebaki Katika dunia hii ni dhiki kuu ya mpinga Kristo na mapigo ya Mungu,si siku ya kuitamani..

Nyakati hizi ni za kuwa macho sana, mana yapo Mafundisho mengi ya uwongo yaliyozaliwa ndani ya Ukristo,wengi wakiamini hakuna unyakuo wa kanisa, wengine wanaamini wakati huu tunaoishi ndio utawala wa miaka elfu moja, wengine wameenda mbali zaidi wakiamini utawala wa Bwana Yesu umeshapita na tunaishi Katika utawala wa Mungu Baba, na Mafundisho mengine mengi ambayo hayana ukweli wowote kulingana na Biblia..

Sasa Mafundisho kama hayo yamekuwa kama ni donda ndugu, kuwafanya watu walirudie neno la Mungu,inakuwa ni ngumu, hivyo hatuna budi kuwa wasomaji sana wa biblia huku tukimruhusu Roho Mtakatifu atufundishe..

Shalom..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT