Uga ni nini kibiblia?

  Maswali ya Biblia

Uga ni sakafu ambayo hutumika kwa ajili ya kupepetea ngano, au kwa lugha nyingine kupuria ngano, na sehemu hii ilitumikia kipindi cha zamani kama tunavyojua zamani hakukuwa na mashine kama wakati huu hivyo ilikuwa baada tu ya nafaka kutolewa shambani ikiwa pamoja na majani yake moja kwa moja ilipelekwa kwenye hiyo sakafu kwa ajili ya kutoa maganda Katika nafaka ili ibaki ngano tu..

Na sehemu hii uga sakafu ilijengwa kwa kutumia mawe au sehemu ngumu ya ardhi, na hii ilikuwa ni lazima kwa kila mwenye shamba lazima awe sehemu hii maalumu yaani uga kwa ajili ya kupuria nafaka zinatoka shambani na ilikuwa inatakiwa iwe karibu na shamba, na sehemu hii katika biblia imepatikana katika kitabu cha

 Ruthu 3:1 “Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema?

2 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani.

3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa”.

Sasa baada ya nafaka kutolewa shambani na kuwekwa katika uga, baada ya hapo walichukuliwa wanyama, mfano punda, ng’ombe nk.. walipitishwa katikati nafaka ili waweze kukanyaga ili yale maganda yaliyo katika nafaka yatoke ili na ibaki nafaka halisi, kwahiyo kwa kitendo hicho cha wanyama kupita juu yake ilifanya yale maganda yalegee.

Baada ya hatua hiyo kumalizika hatua iliyofuata ilikuwa ni haya maganda yaani makapi kuondolewa na kubaki sasa nafaka halisi, kwahiyo yalipeperushwa kwa kutumia kifaa maalumu kilichoitwa pepeto, pepeto lililotumika wakati ule, halikuwa kama hili la kwetu, la chekecheke, hapana, bali lilikuwa ni beleshi fulani ambalo mbeleni lina mdomo kama wa uma au rato hivyo kupitia kifaa hicho walichofanya walikuwa wanakipitisha katikati ya hizo nafaka ambazo tayari zimeshakwisha kukanyangwa na ng’ombe, pale kwenye uga, kwahiyo baada ya kupitisha katikati wanarusha juu, ili kufanya yale makapi yapeperushwe na upepo na ili nafaka ibaki bila uchafu, walifanya hivyo mara nyingi zaidi hadi pale nafaka ilipo baki yenyewe pasipo haya maganda au makapi chini kwenye uga

Na baada ya zoezi hilo kuisha walichota hiyo nafaka na kwenda kwenda kusaga ikiwa tayari kabisa kwa matumizi ya chakula nyumbani

Kwahiyo kazi kuu ya uga ilikuwa ni hiyo, Je kupitia sehemu hii ya uga kuna jambo la kujifunza nasi katika maisha yetu ya rohoni?

Jibu ni ndiyo:

Tukisoma maandiko katika mathayo neno la Mungu linasema

Mathayo 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika”.

Jambo linaloendelea sasa katika ulimwengubwa Roho ni Bwana Yesu kulisafisha kanisa lake na sisi ndiyo nafaka na tupo katika sakafu hiyo yaani uga ambapo hapo sasa Bwana ameshika pepeto lake mkoni kisha anarusha rusha ili kuruhusu ngano halisi ibaki, sasa ikiwa upo katika kundi la makapi ni rahisi sana kuchukuliwa na upepo

Na neno la Mungu linasema baada ya hapo hayo makapi yatachukuliwa na kuchomwa moto.

Kwa kulijua hili lazima tuwe makini ili kuepuka, na jambo la kuepuka hapo ni huo upepo, pepo sasa hivi zipo nyingi ambazo zinafanya watu wapeperushwe pasipo wao kijitambua, mfano upepo wa mafundisho ya uongo, fedha, anasa, uzinzi nk, haya yote ikiwa mtu ujaimalishwa na Bwana Yesu ni rahisi na vyepesi kupeperushwa, na zaidi usipo kuwa makini katika mafundisho nako pia utapeperishwa ikiwa kila siku unasikia injili ya kubembelezwa tu unaambiwa ishi tu utakavyo maana umesha samehewa milele kwahiyo ishi vyovyote tu injili kama hizo ni Moja ya upepo tena si upepo tu ni kumbunga kikali, Iwe makini nano la Mungu linasema Imani bila matendo imekufa sasa kwanini ufundishwe uongo mzito hivyo Tunahitaji msaada ili tubaki salama.

Hakuna msaada mwingine au pengine zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwake ndiyo tunayapata yote maana kukimpokea yeye tunafananishwa na mtu akili

Luka 6:47-49

[47]Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake.

[48]Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.

[49]Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.

Ikiwa Leo ujampokea Yesu Kristo maishani mwako fanya hivyo ili uwe imara usichukuliwe na upepo wa aina yeyote.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT