Kuhadaa ni neno lenye maana ya kudanganya au kulaghai, kuhadaa ni kutumia njia ya mkato au isiyo sahihi ili kuweza kufanikisha jambo fulani au kulipata..
Tunaliona neno hili kwenye baadhi ya vifungu..
Mwanzo 31:20[20]Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia.
Mithali 12:5[5]Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.
Warumi 1:28-29[28]Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
[29]Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
2 Petro 2:14[14]wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana.,
[18]Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
Kuna mifano halisi ya kuhadaa.,
>>>>Ikiwa uko kwenye ndoa, ukachukua hatua yakwenda kwenye anasa za kumbi za starehe na kufanya uzinzi na Wanawake wanaojiuza, huku nyumbani umemwaga mwenza wako kuwa umesafiri kikazi, hapo umehadaa..
>>>Kama wewe ni mfanyabiashara na unadesturi ya kupunguza uzito wa jiwe la kupimia ili ufanye kipimo cha mteja kuwa kidogo kwa bei hiyo hiyo,au unapopandisha bei tofauti na ile iliyo elekezi,huko ni kuhadaa..
>>>> Kutumia vipawa vya Mungu vilivyo ndani yako, kwa lengo la kupata maslahi fulani Katika utumishi, wewe ni nabii,unatoa unabii kwa mtu nakumwambia Mungu ameniambia utoe kiasi fulani cha pesa ili upokee baraka kutoka kwangu na ukifahamu kabisa tumeambiwa tutoe bure kwasababu tulipewa bure hapo umehadaa
Tabia hii ya kuhadaa inatoka moja kwa moja kwa shetani, kwasababu ndiyo tabia yake, tokea mwanzo pale edeni,tunaona aliitumia kumuhadaa hawa na kumuaminisha atakuwa kama Mungu akila matunda ya mti wa ujuzi wa mema mabaya,kumbe sivyo..
Maandiko yanasema shetani ni baba wa uwongo,ikiwa na sisi tabia hii ya kudaa ikitoka ndani yetu basi tufahamu tunadhihirisha tabia hii ya shetani, kuhadaa kunatokana na wivu, chuki za kutopenda wengine waendelee na kufanikiwa..
Tukitafuta kwa bidii kuwa na upendo wa Mungu ndani yetu,tabia ya kuhadaa itakufa ndani ya mioyo yetu na tutajivika pendo..
Yesu Kristo pekee ndiye mwenye uwezo,ndiye tiba pekee atakusaidia…
Shalom…
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.