UPAKO NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Upako ni Uweza wa kipekee wa Roho Mtakatifu ambao huwa huingia ndani ya mtu, ili kumsaidia kufanya jambo fulani kirahisi zaidi, au anakuwa na uwezo wa kutenda jambo ambalo hapo kabla alikuwa haliwezi kulifanya kwa urahisi.

Zamani kibiblia, mtu kabla hajatawadhwa kuwa mfalme, ilikiwa ni lazima itie mafuta, ikiwa na ishara kwamba, mafutwa yaliyomwagwa ndani ya roho yake yanakuwa kama Baraka kutoka kwa Mungu, yanayomsaidia yeye kuwa mtawala
(Pitia kifungu hiki 2 wafalme 9:6)

Pia hiyo ilikuwa kwa watumishi wa Mungu mfano kama makuhani, na manabii, hata nao pia walikuwa wanatiwa mafuta kabla ya kuanza kuifanya kazi ya Mungu.
(Kutoka 29:7)

Lakini upako katika agano jipya vipo vigezo ambavyo ni lazima vifuatwe hili kutiwa mafuta
Na vigezo hivi havitegemei kumiminiwa mafuta ya aina yoyote ndani ya mtu, bali hapa mtu anapokea upako (mafuta) kwa kutenda maagizo ya Mungu..

Waebrania 1:8-9
[8]Lakini kwa habari za Mwana asema,
Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;
Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

[9]Umependa haki, umechukia maasi;
Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,
Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Hapa tunamwona BWANA WETU YESU KRISTO, ambaye Mungu alimtia mafuta (upako) mwingi zaidi kuliko watu wote kwa sababu, waliowahi kuishi duniani, Bwana Yesu mafuta yalikuja juu yake kwa sababu moja … Kwasababua alipenda haki na akauchukia ubaya (maasi).

Inadhihirisha kabisa hakuna upako hauji kwa njia ambazo tunazotazamia sisi, kwamba ukitaka upako ni kwenda milimani kufunga na kuomba sana, au kuwekewa mkono na Mtumishi fulani, hii si sawa, ni vyema kweli tukafanya hivyo lakini je katika kufanya hayo yote, huku nyuma tunampendeza Mungu? Matendo yetu yanamwakilisha Mungu?, Lakini endapo hatufanyi hayo na huku tunatafuta mafuta ya Roho mtakatifu upako, hapo tuwe na uhakika kabiasa kazi inayofanyika ni bure hakuna chochote.

Vipo vigezo vya kupoke UPAKO, ni muhimu na ni lazima kwanza tujazwe Roho, si kwa kunena kwa lugha, bali hapa ni kwa kutii NENO LA MUNGU, kama alivyofanya Bwana wetu Yesu Kristi, kwa kutopenda uovu alijazwa UPAKO

Na sisi hivyo hivyo kama tukitii agizo la Mungu hapo ndipo tunaruhusu NGUVU KUBWA YA UPAKO KIJAA NDAN YETU

Basi tambua hili ikiwa huna Roho Mtakatifu ndani yako, kamwe huwezi, kupokea nguvu ya kufanya jambo lolote , maan hutoweza kuelewa neno la Mungu maandiko, huwezi kushinda dhambi hata pia huwezi kwenda mbinguni hata kama ulipambana kiasi gani, kama huna Roho wa Bwama ni bure.

Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Lakini ikiwa utapenda Bwana akupe kipawa hicho, basi fahamu kuwa kipawa hicho ni bure,,, na wala hakiihitaji kutumia nguvu kukipata..Jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kutubu kwanza kwa  kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote,, kisha ukishatubu sasa na kusema kuanzia leo, mimi na ulimwengu basi, na kuanza kumtazama Kristo,. na kutaka kujifunza Neno lake kwa bidii..Mungu akishaona umegeuka na kuacha uliyokuwa unayafanya basi atakusamehe,. na AMANI YA AJABU itaingia ndani yako..Na yeye atasimama kukusaidia kwa namna ambayo hujawahi kuiona katika maisha yako.

Tafuta ubatizo:
Kisha bila kupoteza muda nenda katafute mahali utakapobatizwa katika ubatizo sahihi.. wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la YESU KRISTO,. sawasawa na (Matendo 2:38) ili uukamilishe wokovu wako, na kumruhusu Roho Mtakatifu kuingia ndani yako, na kuweka makao yake milele ndani yako..

Ukishafanya hivyo kwa moyo wa dhati bila kigugumizi, basi fahamu kuwa Roho wa Kristo ameshaingia ndani yako,. muda mfupi baadaye atakushushia vipawa vyake., kwa jinsi apendavyo yeye, aidha lugha, aidha maono, aidha ndoto, aidha uinjilisti,au unabii n.k.. Wewe tu mwenyewe utaona badiliko ndani yako siku baada ya siku..atakuwa anakufundisha na kukuongoza katika njia ya kweli yote, kwasababu yale mafuta yake tayari ameshayamwaga ndani yako.

1Yohana 2: 27 “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote., tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.

Hivyo atakufundisha, na kukupa upako halisi unaotoka kwake, na sio ule feki unaouzwa na manabii wa uongo katika chupa,. na vifungashio mabarabarani, upako unaotoka kuzimu, usioweza kuyageuza maisha yako.

Fanya hivyo, Na Bwana akusaidie katika kukamilisha hatua zote hizi.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ + 225789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *